KHOFH

MPANGO WA MUNGU

MPANGO WA MUNGU
NA
WAEMA J. MUTULU
UTANGULIZI
Maisha ya leo yamejaa matatizo ambayo, chanzo na sababu zake hazieleweki. Watu ni wenye chuki, hasira, na mabishano huku kila mmoja akitaka kulingana na fikira zake; magonjwa, vita, na mauaji yatokanao na tetemeko za ardhi, vipunga vikali, mafuriko na vita yamejaa kila mahali.
Je, ni kitu gani kinasababisha hayo yote. Ikiwa kuna Mungu aliye muumba na mwenye mamlaka juu ya vyote, kwa nini anawachilia haya maovu? Kwani yalianzia wapi na yataendelea hata lini? Kuna jambo lolote mwanadamu anaweza kufanya akaleta suluhusho? Kitabu hiki kinaeleza kwa ndani maana ya hayo yote na ule mpango wa Mungu ambao atautumia kuleta
suluhisho.
Ni ombi langu kwamba, wote watakaosoma huu ujumbe watauelewa na kusaidika katika maisha yao, ikiwa watakubali
na kuamini.