KHOFH

January 30, 2007

VOICE IN THE WILDERNESS CHURCH OF GOD

January 30, 2007

Salamu Wandugu,

Ni tumaini langu kuwa hii barua itawapata mkiendelea kung’ang’ania kumcha Mungu na kuzishika anri zake kama vile tunavyo…. amrishwa katika bibilia. Maisha hapa marekani yanaendelea siku baada ya nyingine huku watu wengi wakiendelea kuweka akili na mioyo yao katika mali. Ni wachache sana ambao wanamfikiria Mungu na maisha yake.

Watu, na ata wengine wa kanisa la Mungu wamejiingiza kwenye masumbuko ya ulimwengu huu. Wakati Bwana na Mwokosi wetu alijaribiwa na shetani huko jangwani kwa njia ya chakula, alimwambia,”Mtu aishi kwa mkate peke yake, mbali kwa kali neno itakalo kinywani mwa Mungu – mat 4:4.

Wandugu, neno la Mungu (chakula cha kweli kiletacho usima wa milele) imeandikwa katika bibilia. Ni kupitia kwa neno la kweli iliyoandikwa hapo ndani, tunatakaswa na kutengwa na ulimwengu – Yohana 17:17. Bwana wetu anazidi kutueleza katika 2 Wathes 2:15” kwa hivyo wandugu, simameni imara, na kushikilia sana mafundisho mlioyapokea, iwe ni kwa neno au kwa barua zetu”. Tunaambiwa tushikilia sana tamaduni tulisozipokea. Lakini, ni tamaduni gani, ambazo bwana anaongea juu yake?

Kumekuwa na mila katika kanisa la Mungu siku hizi ya kufuata kalenda ya wayahudi, kuamua siku za sikukuu za Mungu. Je, hii ni baadhi ya zile tamaduni ambazo Bwana ametuambia tushikilie?

Je, kalenda ya wayahudi imepangwa kufuatana na neno la Mungu katika Biblia? Hili somo, nimeileta kwa sababu, wengi wamekuwa wakiniuliza kuhusu nyakati za sikukuu mwaka huu. Sikukuu Mungu alizotuamrisha ni za muhimu na haziwezi chukuliwa tu kwa urahisi.

Kwa hivyo, ili tuweze kuwa na uthabiti, hebu tujadili mambo kadha hapa. Mungu anatuambia katika 2 Tim3:16, kwamba “kila andiko limekuja kwa ufunuo wa Mungu, na linafaa kwa mafundisho, marekebisho, kurudi na maagizo katika haki” basi, hebu tufuate haya maandiko tuone kama yanakubaliana na mpango wa kalenda ya wayahudi.

Kwanza, hebu tuongee kidogo kuhusu mila. Wakati bwana anatuambia tusimame imara na kushikilia sana mila,tunashikilia za wanadamu au zile za Mungu katika biblia? Bwana anaonyesha vizuri sana kuwa ni mila za neno, ambayo ni Yesu katika biblia – ona Yohana 1:12. hizi mila ni maandiko matakatifu.

Kwa hivyo, ikiwa mpango wa kalenda ya wayahudi ni wa kweli, unafaa kuonekana mahali katika bibilia maana, kweli yote inaweza kuthibitishwa na biblia kama ni kweli. Tunapaswa kuwa na ufahamu mkamilivu wa biblia, kuhusu wakati sikukuu za Bwana zinafaa kutunzwa. Kwa hivyo, hebu tuone vile vifungu katika biblia ambavyo vinaongea kuhusu hizi sikukuu. Kwa wale wanataka undani wa hili jambo, tunao ujumbe. katika hii barua, tutaeleza juu juu tu.

Mungu ameonyesha vizuri sana katika biblia wakati sikukuu zake zinafaa kutunzwa. Tukifuata biblia, hatutajikuta tikipotoka kama wengi wanavyofanya kwa kufuata mpango wa kalenda ya wayahudi. Biblia haijaagiza watu kubadilisha hizo nyakati. Mungu peke yake ndiye anaweza kutakasa siku na kuifanya halali.

Hapa, nataka kuonyesha kwa uchache vile tunaweza kuelewa na kuhesabu ata tufikie siku za kutunza sikukuu za Mungu kulingana na mandiko. Ona 2 wak 11:3; 2Tim2:15; luka 10:21. Kumbukeni, kuelewa kuzuri kunatokana na mtu kutii amri za Mungu kwa kuzitenda – ona Zab 111:10. katika mwanzo 1:14, Mungu anasema aliziumba na kutupatia jua,mwezi, na nyota, kutufahamisha miaka miezi, siku, eee nyakati. Halafu, katika walawi 23, tunaona orodha ya sikukuu zake na tarehe zake za kuzitunza. Siku ya kwanza ni sabato ya wiki, halafu zile zingine zinafuata. Zote tunajua kwamba, jua likitua, siku moja inaisha na nyngine inaanza.

Ili tuweze kujua nyakati za hizi sikukuu, tunapaswa kufahamu wakati mwezi unaisha na mwingine unaanza. Tukiisha jua wakati mwezi unaisha na mwingine unaanza, itakuwa ni rahisi kujua ile tarehe sikikuu Fulani itakuwa. Tumeamrishwa kuitunza pasaka tarehe 14 ya mwezi wa kwanza wa mwaka, na tarehe 15 mwezi huo huo, kwa siku saba iwe sikukuu ya mikate isiyo chachwa.

Mungu alitupa mwezi uwe ukituwezesha kuhesabu miezi, vile jua linatusaidia kuhesabu siku. Neno la kiebrania la mwezi, ni sawa na lile la mwanzo wa mwesi. Hivyo, Mungu alisema,” zugumza na wana wa Israeli, uwaambie, katika mwezi wa saba (mwezi mpya), katika siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na sabato, kusanyiko takatifu – walawi 23:24”. Basi, ikiwa wakati mmoja watu wanaangalia mwandamo wa mwezi mpya kutunza hii sikukuu, na wakati mwingine, kufuatia kalenda ya wayahudi, si hii inakana maandiko na kuleta farakano? Zile sababu watu (sio Mungu) wanatoa kueleza sababu ya kuamisha hiyo sikukuu, ni kuwa, tarehe moja ilifika siku ya ijumaa, hivyo kuleta sabato mbili zilifuatana. Je, Mungu alisema ziwe zikitenganishwa? Hapana. Hii ndiyo inaleta farakano katika kuelewa siku halisi ya hizi sikukuu. Lakini sisi wa kasina la Mungu, hatuna ruhusa kuamisha siku ata kama simefuatana sabato tatu maana Mungu katika neno lake hajatuamrisha hivyo. Ndugu zanguni, siku inakuja ambayo, kila mmoja atasimama mbele ya Bwana. Na ni huyu Bwana ambaye anasema,”hizi ndizo sikukuu zangu ambazo mtazitunza kwa wakati wake – walawi 23:37. Bwana wetu ametuambia wazi kuwa, tutahukumiwa kulingana na vile vitu vimeandikwa katika biblia na mojawapo ni hizi sikukuu zake – ona ufu20:2.

Kwa hivyo ningewaomba tuwe watu wa kuchunguza maandiko na kuthibitisha chochote tufanyacho kama ni agizo la Mungu katika maandiko au ni mila na mipango ya wanadamu. Huwezi kuambia Mungu eti sikikuu zake zilibadilishwa na wayahudi, na ukafuata maana ni watu wake. Kama nilivyosema mwanzo wa barua hii, tunao ujumbe wenye maelezo zaidi juu ya hizi sikikuu. Tungekuomba uisome. Hata hivyo tunazo hizi sikikuu kama zinavyohesabiwa kulingana na biblia, na ndizo hizi tumewatumia. Tumaini langu na ombi ni kwamba, kila mmoja wetu awe mtu wa kuchunguza na kuthibitisha mambo yote katika maandiko – sauti ya yesu.

Ni Ndugu Yenu Katika Kristo

Bill Goff.