KHOFH

AMRI KUMI

AMRI KUMI
KIMETAFSIRIWA NA
WAEMA J. MUTULU

Karibu miaka elfu tatu na mia tano iliyopita, Mungu alimpa Musa amrizake ambazo, kama zingefuatwa, zingeleta amani na furaha katika huu ulimwengu uliojaa shida za kila aina. Hizi baraka zipatikanazo kwa kuzitii hizi amri sio za kufaidi maisha ya kimwili tu, bali na hata yale yajayo katika ufalme wa Mungu, maana Yesu alisema,” … ukitaka kuingia katika uzima,
zishike amri … Mat 19:17-19.”
YALIYOMO

1. Amri kamilifu yenye uhuru
2. Amri ya kwanza
3. Amri ya pili
4. Amri ya tatu
5. Amri ya nne
6. Amri ya tano
7. Amri ya sita
8. Amri ya saba
9. Amri ya nane
10. Amri ya tisa
11. Amri ya kumi
12. Amri mpya
Kitabu hiki kimetolewa kwa kuelimisha umma na kanisa la Mungu. Sio cha kuuza. Kuchapisha hiki kitabu kuliwezeshwa na fungu la kumi na sadaka za waumini, na baadhi ya wasomaji wetu ambao wanaamua kusaidia kufanya hii kazi kwa michango yao. Karibu!
AMRI KAMILIFU YENYE UHURU
Tanaishi katika ulimwengu ambao ni mfungwa wa uoga, hofu, huzuni, kutokuwa na furaha, farakano, fujo na vita. Kila siku, tunaona ongezeko la kuvunjika kwa ndoa, watumiaji wa madawa ya kulevya, udanganyifu na wizi, huku mauwaji, unajisi na watoto wakimbizi yakizidi. Uongo na hatari kutokana na silaha ziwezazo kumaliza ulimwengu zimewakaba watu.
Sasa, hebu jaribu kufikiria juu ya ulimwengu bila haya matatizo yoye – eee, ulimwengu uliowekwa huru. Unaona kana ni jambo lisilowezekana? Mungu wa mbinguni aliye muumba wa vyote alimpa Musa suluhisho la haya matatizo yote. Hilo suluhisho ni amri zake kumi. Shida ulionazo leo zimetokana na kuvunuwa kwa hizi amri.kuvunjwa kwa hizi ndiko kunaitwa dhambi, maana imeandikwa; “ kila afanyaye dhambi utenda uasi, kwa kuwa
dhambi ni uasi (uvunjifu wa sheri)- 1Yohana3:4”.
Amri za Mungu peke yake ndizo kamilifu. Nje ya hizo amri ni yale maisha ya shida unayaona sasa. Ajabu ni kwamba, tunaona na kusikia wakristo wakisema eti hizi amri zilitupiliwa mbali
na Yesu alipoangikwa msalabani. Lakini tukisoma biblia kinyume cha huo usemi, Mungu anasema; “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye nimenjua na wala hazishiki amri zake ni mwongo na kweli haimo ndani yake – 1Yoh2:3-4”. Ukweli ni kwamba, walimwengu wakijawa na roho ya shetani hawataki kuagizwa vile watafanya na yeyote yule. Wanataka waenende kivyao (War8:7).
Wengi wa wakristo usema kuwa amri kumi ni mila za wayahudi, wengine ufikiria ni za agano la kale na hazituhusu sisi tulio wa agano jipya. Baadhi ya wengine, huku wakitumia biblia vibaya usema ni ngumu na ndiyo sababu Yesu aliziondoa. Lakini Yesu mwenyewe alisema,” … wala amri zake sio nzito “ na tena, “ kwa maana nira yangu ni laini, na mzingo wangu ni mwepesi – 1 Yoha 5:3; Mat 11:30. ni amri za kukuweka huru.
JE, AMRI KUMI ZIL lTUPILIWA MBALI
Wengi ufikiria kuwa Musa ndiye aliwapa wa – Israeli amri kumi. Lakini sio hivyo. Mungu mwenyewe ndiye alizitoa kwa ngurumo na radi huko mlima Sinai, na akaziandika kwa kidole chake mwenyewe juu ya mawe, kisha akampa Musa (ona Kutoka 20:1;31:34;34:1).
Na ukitaka kujua hasa yule Mungu alitoa hizi amri, utakuta kwamba ni Yesu maana alipokuja duniani miaka mingi baada ya Mungu kutoa hizi amri, alisema; “ Naye baba aliyenipeleka …
Sauti yake hamkuisikia wakati wowote – Yoha5:37”. Yule Bwana aliyezitoa hizi anaitwa”MWAMBA” (ona – Kumbukumbu la torati 32:4).
Kulingana na agano jipya, huyu mwamba ni Yesu (ona 1 wakor10”4). Yesu tangu mwanzo ndiye yule neno aliyekuwa kwa Mungu. Ndiye tangu mwanzo amekuwa akihusiana na
mwanadamu. Wengi hudhania kuwa amri kumi zilianza na agano la kale; lakini Mungu anasema,” … Ibrahimu alitii sauti yangu na kuzishika amri … zangu- Mwa 26:5”. Hii inaonyesha wasi kwamba amri za Mungu zilikuwa hata kabla ya agano la sinai.
Amri za Mungu ni maisha yake. Kwa hivyo, zimekuwa tangu milele kama Mungu mwenyewe (soma Zab 119:172; 89;111:7-8). Hii ndiyo sababu Yesu alisema; “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza (kuishi kwa kuzifuatia). Maana amini nawaambieni, ni rahisi mbingu na nchi kupita kuliko nukta moja ya torati kutanguka. Basi yeyote atakayevunja amri moja kati ya hizi … na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo katika ufalme wa Mungu… Mat 5:17-19. Kudhibitisha usemi wake, alipomjia kijana akitaka kujua namna ya kuurithi uzima wa milele, Yesu alimwambia;” … ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri Mat5:17-19.
Yesu alimwambia; “Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtatenda yale ninayowaambia – Yoha15:14”. Kwa hivyo, yeyote yule anaejiita mfuasi wa Yesu, Yesu anamwambia, “ZISHIKE AMRI “ Mat 19:17.
Mungu uwapa wafuasi wa Yesu roho yake takatifu ili, “ maagizo ya torati yatimizwe ndani yao … Waru 8:4”. Maana aliahidi kwa kinywa cha nabii Ezekieli; “ Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaongoza katika sheria zangu, nanyi mtazitii, na kuzitenda – Ezek36:27”. Ona pia 1 Wakor 7:19. nasema nini? Wakristo wa kweli ambao ndio kanisa la Mungu wanazishika amri zote kumi za Mungu (Ufunuo 12:17; 14:12). Ona pia Ufunuo 22:14; Mhubiri 12:13.
Hizi amri za Mungu ni za kiroho na, sio vile wenye akili ya kimwili ufikiria (soma Warumi7:12,14). Katika hivyo vifungu vyote, hatujaona hata kimoja kikiongea juu ya kuondolewa kwa amri kumi. Hii ni kwa sababu,” amri zake zote ni za haki … zimethibitika milele na milele- Zab 111:7-8”. Ona pia Isa 51:6. fundisho lolote nje ya haya maelezo ni ya uongo na haitokani na Mungu, maana yeye utuagiza tuzishike amri zake.
Hata hivyo, kwa uwezo wetu, hatuwezi kuzitii maana ni za kiroho, huku sisi tukiwa wa kimwili (ona Warumi 8:7,6; 1 Wakor 2:14. hapa ndipo neema ya Mungu iliyo katika kristo inaingilia. Dhambi ni kuvunja sheria za Mungu. Kwa neema ya Yesu, macho yetu ufunguliwa (ona 2 Wakor4:6). Tunapoelewa vitendo vyetu vya uvunjaji wa hizi amri, Yesu atuagiza akisema;” Tubuni …. Matendo 2:38”. Kwa maana nyingine, baada kupewa kuona dhambi zetu, ni lazima tugeuke; tufanye agano na muumba wetu ya kutovunja amri zake tena, na kuamini kwamba hizi amri ndizo maisha ya kweli. Papo hapo, kama anavyoeleza petro, baada ya kubatizwa na kuwekelewa mikono, Mungu utupa roho yake (Matendo 2:38) ili ituwezeshe kuzishika amri hizi za kiroho na sio ya kuzitupilia mbali (soma War 3:31;6:1). Sio
kwamba, baada ya kupokea roho ya Mungu tunamiliki mara hiyo; hapa; ni lazima tukue hatua kwa hatua (ona 2 petro3:18). Agiza pia kitabu chetu kiitwacho,” WONGOFU WA
KWELI”. Kina maelezo zaidi.
Kwa hivyo, amri za Mungu ni maelezo yake kwa mwanadamu juu ya yale maisha ambayo ni ya kweli na makamilifu, na ndizo hasa maisha ya mkristo. Mtu awaye yote asiyezitii hizi amri sio mkristo (soma 1 Yohana 2:2-6; 3:7-8).
AMRI YA UPENDO NA UHURU
Utasikia waalimu wa uongo wakisema;” Tunaitaji kusizitizia uhusiano na sio sheria, ee – tunaitaji upendo na sio amri”. Lakini, umewahi kuelewa kwamba hakuna uhusiano au ushirikiano uwezekanao pasipo sheria? Maana, kama hakuna sheria zinazoeleza vile watu watahusiana, basi huo uhusianao hautawezekana. Pia upendo wa kweli hauwezekani nje ya amri ya Mungu. Hii ni kwa sababu, “kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake, na amri zake si nzito – 1 Yohana 5:3”.
Rafiki zanguni, upendo ndio yale maisha Mungu anaishi, na ambayo wote wampendao huishi kwayo; nayo uelezwa kwa njia ya amri zake- Ona 1 Yohana 4:8, 16. wakati mafarisayo walijaribu kumtega Yesu kwa kumuuliza amri iliyo kuu, Yesu aliwajibu; “Mpende Bwana kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote – Mat 22: 36-37”. Kama utakubali, yesu aliiongea juu ya amri kumi (soma Mat 22:36-40, na ufananishe na kumbukumbu la torati 6:5; Walawi 19:18). Kwa njia nyingine, Yesu alionyesha kuwa, amri kumi na manabii zinafundisha upendo. Kwa hivyo, ukitaka upendo, ni lazima uzishike amri kumi, maana, nne za kwanza ni upendo kwa Mungu, huku sita za mwisho zikiwa ni upendo kwa mtu na mwenzake. Mtu yeyote afundishaye kuwa zimeondolewa na hasifahi kushikwa ni muongo.
Yakubu alielewa hayo tunayosema vizuri sana maana anasema kuwa hizi amri kumi ni kamilifu na za kufanya mtu awe huru (soma Yakubu 1:25). Yesu pia alisema kuwa yeyote ajuaye hii kweli (amri) ambayo ni neno la Mungu (soma Yohana 17:17) itamweka huru – Ona Yohana 8:32. yakubu aliendelea kuonya akisema, “ maana mtu akiishika sheria yote, kisha akosee neno moja tu, atakuwa amekosea yote. Kwa sababu, yeye aliye -sema,” Usizini pia alisema usiue. Basi ikiwa ujasini lakini unaua, wewe umekuwa mvunjaji wa sheria. Basi, semeni na kutenda kama watu wataohukumiwa kwa sheria ya uhuru- Yakubu 2:10-12.
Hivyo basi, kutoka kwa maandiko, mara nne tumeona amri za Mungu zikiitwa sheria ya uhuru na sio, ngumu ya kumfanya mtu kuwa mtumwa vile manabii wa uongo wafundishavyo. Amri za Mungu ni za kukuelekeza kwa njia ya furaha na amani, na kukupatia maisha marefu maana imeandikwa;”Zitakuongezea wingi wa siku, na miaka ya uzima na amani – Mithali 3:2,4:22. daudi akielewa haya, alisema; “Nami nitatii sheria yako daima,
naam, milele na milele. Nami nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza amri zako – Zab119:44-45.”
AMRI ZA KIROHO KWA WATU WOTE
AMRI KUMI NI MAISHA YA
Mungu yakielezwa kwa njia ya hizi pointi kumi. Kwa vile
aliumba mwanadamu kwa sura yake na mfano wake, alikusudia huyu mwanadamu aishi kwa hayo maisha yake. Kwa sababu hii, alimwandikia kwa ufupi kwa njia ya hizi amri kumi.
Vifungu vingine vyote katika biblia vimetokana ni hizi amri kumi- eee, biblia ni ufafanusi wa hizi amri (Zab119:96). Hizi amri kumi sio maelezo ya kimwili bali, kwa vile ni maisha ya Mungu aliye roho, ni lazima yawe ya kiroho; maana imeandikwa; “ Twajua torati asili yake ni ya rohoni … Warumi 7:14”. Isaya akitabiri kuhuzu hizi amri alisaema kuwa, Yesu atafafanua – ona Isaya 42:21. kwa kweli, Yesu alizifafanua maana ukisoma ujumbe wa mlimani katika Mat 5:1; 7:29, utaona akionyesha hizi amri kwa njia ya kimwili na pia ya kiroho (ona Mat 5:21-22,27-28).
Hapa katika kuzifafanua, Yesu alionyesha vile hizi amri zitageuza mawazo yetu- rohoni na sio matendo yetu peke yake. Kama unataka kuelewa, hizi amri ndizo msingi wa ufalme wa Mungu na ni za wote watakaourithi. Mungu akishuhudia hayo alisema; “Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi- Hesabu 15:16”. Ona pia Isaya 56:6-7.
Atakapokuja Yesu na kuanza utawala wake hapa duniani, maandiko yanasema juu ya hizi amri, “Maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno katika Yelusalemu – Isaya 2:3”. Wote, wayahudi kwa wamataifa, walio katika Kristo- yaani, wakristo uishi kwa kufuatia hizi sheria ambazo ndizo neno la Mungu katika biblia. Ni kosa kubwa Mkristo yeyote kufikiria eti hizi amri ni za wayahudi na hazina maana kwake. Yesu anakuambia; ”Ukinipenda utazishika amri zangu na tena,” Haya maneno niyasemayo si yangu bali, ni ya baba aliyenituma- Yohana
14:15;12:49”. Eee, amri za Yesu ni zile za Mungu na ndizo hizi tunazungumzia hapa.
AMRI YA KWANZA
Wana wa Israeli waliposimama mbele ya mlima Sinai wakati Mungu alikuwa akitoa hizi amri kumi, uwezo wa Mungu ulidhihirika kwao huku mlima ukiyumbayumba, na ngurumo
na radi zikionekana (ona Kutoka 19:16-18; Zab18:13). Ndipo Bwana akawaambia; “Mimi ndimi Bwana Mungu wenu aliyewatoa nchi ya Misiri- Kutoka 20:1-2; Kumbukumbu 5:6”.
Ndio uelewe vizuri kuwa hizi amri ni za wakristo wote, Paulo katika Waebrania anafananisha vile wa-lsraeli walisimama mbele za Mungu kwa njia ya kimwili- soma Waebrania 12:18-21-
kuhusu Israeli huko sinai na, Webr 12:22-25- kuhusu kanisa la Wakristo mbele ya kiti cha enzi cha Mungu cha mbinguni. Kwa hivyo tunapoendelea kusoma hizi amri moja moja, usisome kama maneno ya Mungu kwa wa-Isaeli bali, kama sauti ya Mungu akiongea na wewe.
Mungu ndiye muumba wa vyote na, ana hukumu juu ya vitu vyote, maana imeandikwa;” Kwa hukumu zako vitu vimesimama imara hata wa leo; maana vitu vyote ni watumishi wako- Zab119:91”. Mungu ueleza uwezo, nguvu na hekima zake kwa njia ya matendo yake. Akionyesha wa-lsaeli ni kwa nini wanapaswa kumwabudu, aliwakumbusha vile aliwatoa utumwani; yale maajabu alitenda mbele ya Ferao; Aliamrisha maji katika bahari ya shamu yakatoa njia; Akawapa maji na chakula huko janawani.
Ukisoma katika biblia, utaona vile Misri ni mfano wa ulimwengu na Ferao ni mafano wa shetani. Kwa huu mfano wa wa-Iraeli, Mungu anawaambia wanadamu wote, vile katika Kristo Yesu aliwatoa ulimwenguni, vile ndiye aliyewaumba, anawakumbusha vile maisha yake ni mazuri na yenye amani na ndiyo yanapaswa kufuatwa. Hii ndiyo sababu Yesu alisema;”Ukitaka kuingia uzimani (katika ufalme wa Mungu), zishike amri. Kijana akamuuliza; “zipi – Mat19:17-19? Hii inatulete katika amri ya kwanza.
USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI
WAKATI Mungu aliwapa wana-israeli amri zake, ulimwengu wote ulikuwa ukiabudu miungu ya sanamu. Wa-israeli walikuwa wametoka Misri ambako miungu ya huko ilikuwa ni Osiri na Isi, na pia, Ferao aliabudiwa kama Mungu katika dunia. Kwa hivyo, kabla wa -Israeli hawajafika Kanaani, nchi yenye ibada za sanamu, mbaya kushinda zile za Misri, Mungu alianza kuwafundisha vile ibada zake ufanywa, kwa kuwapa amri zake. Aliwaamuru wasiabudu miungu mingine, maana Bwana ambaye jina lake ni wivu, ni Mungu mwenye wivu – Kutoka 34:4”. Je, hapa Mungu alikuwa akitaka sifa na kutukuzwa, ama nikitu gani
anaonea wivu?.
Sio kwamba Mungu anajitakia. Ijapokuwa kwa hakika, yeye ni mkuu, kile kitu anachukia kuhusu hii miungu ya sanamu ni yale maisha watu wanalazimika kuishi. Maana walikuwa, na hata wa leo wote waabuduo sanamu wanalazimika hata kuua watoto wao (ona kumbukumbu 12:13), Watu ambao Mungu amewaumba kwa sura yake. Ukweli ni kwamba, ibada za sanamu ukiwemo ukristo wa uongo zimeumiza watu duniani na kuwapa maisha
magumu na ya uharibifu. Kama kila mtu angefuata maagizo ya mumba wake ambayo peke yake ndiyo yanaeleza ibada ya kweli, ulimwengu ungekuwa na amani kuu, maana huyu muumba na maisha yake, ni upendo. Mungu haoni wivu kwa ajili yake bali, kwa kule kukutakia maisha mazuri.
Watu duniani wana kila aina ya ibada. Baadhi ya watu huamini Mungu anaishi mlimani, wengine chini ya miti mirefu. Wengine ufikiria wanyama fulani kuwa Mungu, wengine sanamu za wanawake; Ndege fulani uchukuliwa na wengine kama Mungu, na mengine mengi. Hizi ibada zote na asili yake ni shetani maana haziimarishi, bali zinaharibu maisha kwa njia moja au nyingine. Hii ndiyo sababu biblia inasema;”Vitu vyote watoavyo sadaka (kwa ibada) wavitoa kwa mashetani sio kwa Mungu… ninyi msishirikiane na mashetani – 1 wakor10:20”. Kwa hivyo, mtu yeyote anayeasi maagizo ya Mungu uabudu mashetani. Mungu anawaagiza wote wamwabuduo akisema;” Msijifunze njia za mataifa……. ushangaa kwa sababu ya hizo- yeremiah 10:2”.
Wakristo leo watasema hawafuati mambo hayo. Jambo wasilolielewa ni kwamba; mafundisho yote ambayo hayako katika biblia, kama siku za krismasi, ista, mwaka mpya;
imani kama za kuenda mbinguni, utatu wa Mungu n.k., zote ni mafundisho ya mashetani na, ni ibada za sanamu (soma kumbukumbu 12:29-32). Yesu alisema, tukifuata mafundisho ya
wanadamu badala ya sheria za Mungu, tutakuwa,”tunamwabudu bure “( soma Marko 7:7-9).
Je, ibada ya sanamu na maagizo ya wanadamu ndiyo kuwa na miungu mingine peke yake? Yesu alisema;” Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake-Matt 4:10”. Paulo aliongezea akishangaa; “hamjui ya kuwa, kwake yeye mjitoao kuwa watumwa kumtii, mmekuwa watumwa wake… kwamba ni utiivu wadhambi uletao mauti au, wa haki uletao uzima- Waru6:16?’.
Wewe, ni kitu gani unatumikia? Unajibidiisha kufikia nini katika maisha yako? Ee, kwa hakika, ni kitu gani unapenda, na hivyo kukitafuta kwa moyo wako wote? Ikiwa kwa kila jambo utafuti kumpendeza Mungu, basi kile unapendeza ndicho Mungu wako, na hivyo, umevunja amri ya kwanza. Maana lengo la haya maisha ya kikristo ni kutafuta mapenzi ya Mungu kwa kila kitu tufanyacho – ni kufikiria, kutenda, na kuongea kama Mungu – ona Waefeso 4: 23-24; soma kumbukumbu 6:4-5; Mat22:37. tukishika hili la kwanza, tutakuwa tumeshika zile zingine zote maana, tutakuwa tukifuata neno la Mungu kwa kila jambo – Eee
kila tutendacho kitakuwa ni maagizo ya Mungu.
TUNAABUDU VITU GANI?
Watu wengi ufikiria matatizo yao yanaweza kuisha ikiwa wanaweza kupata pesa nyingi. Basi wao ujibidiisha kupata pesa kwa njia yoyote ile hata kama haiambatani na sheria za Mungu. Yesu alionyesha pesa (mali) kuwa Mungu mwingine. –Ono Mat 6: 24. Paulo pia alitilia mkazo hilo jambo aliposema; “kila aina ya tamaa ni ibada ya sanamu-wakol 3:5”.
Unaweza kuwa na sanamu ya tabia fulani, ni ubaya, hasira, wivu, usinzi, chuki na kadhalika. Bibilia inaonyesha kwamba, kutegemea chochote cha dunia hii badala ya Mungu ni ibada ya
sanamu(Mungu mwingine) – ona Wafilipi 3:19. Ninaposema chochote ninamaanisha-Watu wakubwa (Zab118:8-9), cheo fulani ama, uwezo ulio nao, na hata kule kutafuta kukubaliwa na uma. Yesu alionya; “Kama mtu akija kwangu naye asimchukie baba, mama ,wanawe, ndugu, na hata nafsi yake mwenyewe,
hawezi kuwa mwanafunzi wangu – Lk 14:26;33”. Ndugu zangu, hii tabia ya kutegemea mipango ama uvumbuzi wa wanadamu kusuluhisha matatizo pia ni Mungu mwingine mbaye amewafanya wanadamu wasione haja ya kuomba na kutegemea Mungu muumba wao (soma wakolo2:8,18). Niseme nini? Mtu akifanya chochote kile ambacho kinakana neno la Mungu, huwa ameanza kuagizwa na Mungu mwingine.
MUNGU AWE WA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO
Jambo la kuhuzunisha ni kwamba, sio watu wengi ambao ufikiria juu ya Mungu. Wao utaja Mungu na kumfikiria wakati wa shida. Wana yule mungu wa mfukoni (pesa) ambaye matatizo yakitokea wanamtoa mara moja. Swala ni hili; Je,pesa utatua matatizo? Kama ingelikuwa inatatua, basi matajiri wangekuwa na amani kuu. Lakini ukweli ni ule tumeona Paulo akieleza (soma 1Tim 6:10). Mungu wa kweli, aliyeumba vyote ndiye angefaa kuwa
tegemeo lako. Maana kama vile tumeona awali, kile unatumikia, kufiria na kutenda wakati wowote ule ndicho unachoabudu. Ikiwa ni Mungu, basi utatimiza maandiko yaliyo katika
Wakolosai3:1-4. Tukijifunza kufuata Mungu katika kila jambo, tutajikuta tunafuata maagizo yake na kuyatumia kuhusiana na wanadamu wenzetu, na hivyo, kudumisha wema mkamilifu.
Ikiwa tutamuiga Yesu mwokozi wetu, bila shaka, hii amri ya kwanza itatimizwa ndani yetu, maana alisema;”Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona baba analitenda . Yohana 5:19.
AMRI YA PILI
Je, Mungu niwa kweli kwako, ama unahitaji kitu mfano wa mtu, mnyama, mlima ili vikutegemeze kwake? Eee, nauliza, unamjua Mungu ama unahitaji vitu vionekanavyo kukujulisha kumjua na hivyo kumwabudu? Amri ya pili inahusiano na zile njia tunatumia
kumwabudu Mungu na yale matokeo zinaleta kwetu na kwa vizazi yetu baada yetu. Amri ya pili inasema; Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu
mbinguni, ama chini duniani, amad majin. Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;. Kutoka 20:4-6. ona pia kumbukumbu 5:8-9.
Hapa, Mungu hakatazi uchongaji wa sanamu za watu ama wanyama kama wengine wanavyofikiria. Mungu anakataza utumiaji wa hizi sanamu kama miungu, au njia ya kuabudu.
Ni kwa nini anakataza? Tangu mwanadamu atengwe na roho ya Mungu pale Edeni, huku akiwa hawezi kuelewa na kujua mambo ya kiroho, amejaribu kutumia vitu vionekanavyo kama njia ya kujaribu kumfikia Mungu asiyemjua (soma Matendo 17:23-24). Ajabu ni hii; Ni kweli kwamba hizi sanamu zinaweza kutusaidia kumjua Mungu ama kumfikia? Sio kweli kwamba hizi sanamu zinatufunga macho na kutuzuia kumwelewa. Wakati wa-israeli
walitengeneza sanamu ya ndama pale jangwani na kusema kuwa ni Mungu, yeye Mungu hakukubaliana nao maana alisema;” wamepotoka upesi na kuicha ile njia niliyowaamuru,
wamejifanyia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu… Kutoka 32:8.
Hakukubaliana nao kuwa ndama ni njia nzuri ya kumuabudu bali, ni njia ya kumuacha – ni mungu mwingine. Mungu ni muumba mwenye hekima, nguvu na mamlaka. Je, wewe mwanadamu
uliyeumbwa naye, unaweza kumuumba? Hebu jiulize si huu ni ujinga ( soma Yeremia 10:3, Zaburi 115:4-8). Hii ni kama kumfanya Mungu kuwa mdogo kuliko mwanadamu, na hivyo
kujifungia kabisa njia ya kufahamu mambo ya kiroho kama alivyoshuhudiia Paulo akisema; “wakijionyesha kuwa wenye hekima, wamekuwa wajinga. Wameubadili utukufu wa Mungu
asiyeharibika kuwa mfano wa sura ya mwanadamu aharibikao, na ya ndege, wanyama na kadhalika. Kwa maana wamebadili kweli kuhusu Mungu kuwa uongo; Kwa kukisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Mungu aishiye milele – warumi 1:22-23, 25”. Ndugu zangu, jitihada yoyote ya kuunda kitu chochote kile, ukijaribu kukitumia kusimamia ibada ya Mungu ni dhambi.
ONYO KUHUSU SANAMU
Mungu aliwaonya wa-israeli (na anakuonya wewe) wasisimamishe kitu chochote ama kutengeza chochote cha kutumika kwa ibada- ona Wala 26:1. Mungu aliwakataza
akiwaambia ;”wala msimwabudu Bwana Mungu kwa njia hiyo – Kumbukumbu 12:4”.
Umewahi kukaa ukafikiria maana ya baadhi ya hizi sanamu? Kwa mfano; unajua maana ya msalaba? Ijapokuwa wengi uivaa na hata wengine kuitumia kama njia ya kumwomba Mungu
wakisema inasimamia Yesu, ukweli ni kwamba, msalaba ni ishara ya miungu wa babeli aitwaye Tamuzi ambaye walimsujudia kama mwokozi wao. Huu msalaba unasimamia ile herufi ya kwanza ya tamuzi- T. Tangu mwanzo, huu msalaba ulitumika kwa kuangika watu wakiuwawa. Kwa hivyo, msalaba haukuanza na Yesu. Ni baadhi ya sanamu za kuchonga ambazo ni machukizo mbele ya Mungu; maana amesema;” sanamu za kuchonga za miungu
yao mtaziteketeza kwa moto. kwa maana ni machukizo kwa Bwana Mungu wako; na machukizo usilete ndani ya nyumba yako. Kumbukumbu 7:22-26”.
Hivyo ndivyo Mungu anavyoonya juu ya sanamu za misalaba, za Maria ama za Yesu na watakatifu wengine- ni sanamu ambazo zinavunja amri ya pili. Hatuwezi kuweka Mungu, ama utakatifu wake katika sanduku ama kwa ukuta kwa njia ya picha au msalaba – haya yote ni machukizo.
KUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI
Yesu alisema, wale wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli Yohana 4:24. lakini, kwa vile watu wengi wamedhania mifano ya sanamu kuhusu Mungu, basi, ibada yao imekua ya bure. Hii mifano imetokana na wanadamu kutonyenyekea mbele za Mungu na kumwabudu vile asemavyo katika neno lake. Wao uwazia kila mtu kwa njia yake vile angependa kuabudu na hivyo kukana ile njia ya pekee ambayo mwongozo wake ni neno la Mungu katika biblia. Huu ndio mwanzo wa ibada ya sanamu. Lakini, kama watu wangejikana na kusoma maandiko huku wakiomba kila wakati, kwa njia ya hayo maandiko, wangemjua Mungu kiasi ambacho hawangeitaji njia nyingineisipokua ya hiyo neno.
Mwanzo wa hiki kitabu, tumeona kuwa Mungu uona wivu kwa ajili yetu. Hii ni kwa sababu, ibada ya sanamu umletee mwanadamu madhara ya kila aina. Inatupasa kuelewa
kwamba Mungu ni mkuu na wa milele na, kama hajatuambia lolote lile, hatuwezi kuishi tukawa na furaha na amani. Neno lake ni maelezo yake kuhusu hayo maisha, na kila aishikaye huwa anamwabudu katika kweli (Yohana4:24; 17:17). Tukikataa kutii hayo maagizo katika maandiko, tutalazimika kutafuta njia zetu na hivyo, kufuata sanamu za kila aina.
NI AMRI IPI?
Wakati wamejaribu hizi amri kwa njia fulani na hivyo, kuondoa hii amri ya pil. Hii imewawezesha kuwa na sanamu za Yesu, msalaba, Maria, n.k. elewa vizuri kuwa kuna aina mbili za ibada za sanamu na ndio sababu Mungu alitoa amri mbili kuhusiana na hizo aina mbili za sanamu. Ya kwanza ( Kutoka 20:3) inakataza kuabudu kitu, ama kutegemea kitu kama vile ungemwabudu na kumtegemea Mungu. Ya pili inakataza kuabudu sanamu kama
njia ya kumfikia Mungu. Kusujudu kitu kama namna ya kumwabudu Mungu wa kweli- (ona Kutoka 20: 4-5). Kwa hivyo, wametimiza unabii wa Danieli aliposema kuhusu hili kanisa;”
Naye atanena maneno kinyume cha yeye aliye juu. Naye ataazimia kubadili majira na sheria-Dan 7:25”. Warumi wailibadili amri ya kumi na kuigawanya mara mbili huku wakiondoa amri
ya pili. Wameitupilia mbali njia ya Mungu ya kuhesabu nyakati – yaani, siku kuanza jioni jua likitua, na kuanza kuhesabu siku zao baada ya saa sita usiku. Hata hivyo, hii haikubadili neno la Mungu maana imeandikwa;” Kila kazi Mungu afanyayo hudumu milele haiwezi kupunguzwa wala kuongezwa. Mhubiri 3:14.
AMRI YA TATU
Kwa kila njia, jina la Mungu usimamia maisha, mawazo, matendo na njia zake za kuhusiana na viumbe vyake. Amri ya tatu basi inahusiana na vile tunatumia hili jina kuhusiana na
maisha, maana imesema; “ Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. Maana Bwana hatamhesabia kuwa hana kosa, mtu alitajaye bure jina lake kutoka 20:7; kumbukumbu5:11.
Hii amri inamaanisha kwamba, mtu akilitaja jina la Mungu kuhusiana na maisha ya ulimwengu huu amekosa. Kila tunapolitaja hili jina, ni lazima tuhakikishe tumelitaja katika
kweli, na katika kicho cha Mungu. Hii haimaanishi, kama wengine wafikiriavyo, kwamba ni lazima hili jina litajwe kwa Kiebrania, kiarabu n.k. Kulitaja jina la Bwana kwa kumcha ni kulitaja katika maisha yake mfano. ELOHIMU umaanisha” Jamii ya Mungu”; YHWH, ama Yahweh – umaanisha,” AISHIYE”; EL -SHADAI- Mungu aiiye mkuu”; Haya majina yote ni njia ya kutueleza Mungu ni kwa maana imeandikwa; ” Nao walijualo jina lako watakutumainia wewe, maana huwaachi kamwe wakutafutao – Zab 9:10″. Kwa hivyo, ikiwa haya majina hayakupi uf ahamu wa utakatifu, ukuu, wema – eee, ikiwa hayaleti maana ya uzuri na faida ya kumtegemea Mungu, basi,
kuyataja kwako ni bure.
Wakati wanafunzi walimwomba Yesu awafundishe kuomba, katika kile leo watu wanaita sala ya Bwana, Yesu aliorodhesha ukuu na uwezo wa Mungu, ndiyo -alilitaja jina la Mungu katika kweli (Luka 11:1). Ukisoma vizuri hilo sala utaona maelezo ya vile Mungu alivyo, maana inaonyesha, Baba aliye juu – Elohimu; Jina lake litukuzwe, ufalme wake uje – El-shadai; mapenzi yako
yatimizwe, utupe leo riziki; utuepushe na maovu … ufalme, uwezo na utukufu ni zako – Yahwe, Elishadai? kwa njia nyingine, Yesu alikuwa anawaambia ( na ndivyo anatuambia) wawe na ufahamu wa yule Mungu wanayemuomba – ambaye ni mkuu, mtakatifu, na mwenye hekima kuishinda vyote, na ndiye rnwenye vyote. Ukiomba bila kumwelewa Mungu kwa njia hii, basi, unalitaja bure jina lake.
KUAPA NA KUCHAFUA
Katika kizazi hiki, utasikia jina la Mungu likitumika kwa kulaani mtu ama kwa kiapo fulani. Utasikia katika jitihada za watu za kutaka k ujionyesha, matamshi kama; ” haki ya Mungu; Ngai,
Nyasae, Yesu” n k, Ikiwa watu hawataji majina ya baba zao ovyo-ovyo, imekuaje jina la Mungu awapeye uhai, kuwalinda na kuwalisha liwe la rahisi na la kuchezea? Wote wafanyao hayo
wanavunja amri ya tatu, ambayo inakataza hayo, maana imeandikwa; ” Wala msilinajlafijina langu takatifu, bali mnitakase katikati yenu, rnaana mimi ndimi Bwana niwatakasaye – Walawi
22:32;”ona pia Kutoka 22:28. Kulitaja jina la Mungu kwa mambo ambayo hayaambatani na maisha yake ni kumtukana. Hata, kujichukua kuwa wewe ni mkristo, hivyo kuenda ukisema mambo ya Mungu na huku unaendelea kutenda na kuishi Maisha ya kimwili ni kumshuhudia Mungu uongo maana imeandikwa; ” Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana -Walawi19:12″
Kutilia mkazo hayo aliyoyanena Mungu, Yesu alisema ” Usiape kabisa, hata kwa mbingu … kwa kitu chochote. Mat 5:34-37, Kwa njia nyingine, ongeeni ukweli na hayo yatatosha. Kama ni
ndiyo iwe tu ndio bila kuongezea mengine – ona pia Yakobo 5:12. Kwa hivyo, jina la Mungu ni takatifu kiasi ambacho, haliwezi kutumika kuthibitisha mambo ya wanadamu. Njia la kipekee la
kuapa kwa jina la Mungu ama kulitaja ni kutenda mapenzi yake kwa kutii neno lake, Kwa kufanya hivyo utakuwa unaonyesha watu Mungu, na maisha yake, maana utakuwa unaishi kwa utakatifu wake, ( ona Mat. 5:48; 1 Petro 1:15-16)
Hii ndiyo sababu Paulo anasema kuwa mkristo ni balozi na waki li wa siri za Mungu (ona 2 Wakor 5:20; 1 Wakor 4:1-2). Utaona kuwa, kutaja jina la Mungu katika haki na kweli ni kuishi hayo
maisha yake yanayoelezwa katika biblia, WAONGO NA IBADA ZA BURE Kunao watu wengi leo wanaojionyesha kumwakilisha Mungu na ha li ni waongo. Hawa watu udanganya wengine kuhusu Mungu na maisha yake na ha li wao wenyewe hawamjui (ona Mat. 24:4-5). Hawa pia ulitaja jina la Bwana bure. Watu hawa wameleta mafundisho mengi katika ukristo ambayo ni pembeni tofauti na yale Yesu alifundisha na hivyo, wamefuruga akili za wengi wasielewe maana ya maandiko matakatifu (ona Mat 23:9; Zab111:9; Ufufnuo 19:10; Marko 7:6-8)
Je unataka kujiepusha na kulitaja jina la Mungu? Kama ndiyo, ni lazima ujiepushe na mafundisho na maisha yoyote ambayo asili yake ni ya kibinadamu, na badala yake ujifunze maisha ya Mungu yaliyo katika maandiko (ona Lukas 6:46). Ikiwa tutaita jina la Bwana huku tukiendelea kuishi maisha ya kimwili, itakuwa tunalitaja bure hilo jina takatifu maana imeandikwa;” Sio kila
aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye rnapenzi ya baba yangu …. Wengi wataniambia siku hiyo; Bwana! tulifanya unabii kwa jina lako na kutoa pepo …. . Ndipo nitawaambia; ” Sikuwajua kamwe; Ondokeni kwangu … Rafiki zanguni, kila aiitajalo jina la Mungu na ajiepushe na uovu wa kil a aina, maana wakati wowote tuitaialo katika uovu, huku tukiendelea kuzivun ja amri zake, tutakuwa tunalitaja bure (soma 2 Tim 2:19; 1 Petro 3:10-12).
AMRI YA NNE
Kwa nini ulizaliwa? Maisha yana maana gani? Tunafikia jengo la maisha yetu kwa njia gani? Watu hata hawana nafasi ya kutafuta majibu ya maswali haya kwa muumba wao ambaye ndiye mwanzilishi wa maisha. Hata hivyo yeye yuko tayari kutueleza yote ikiwa tu, tukotayari kusomeshwa naye, Tunahitaji muda fulani wa mapumziko baada ya kazi, kwa ajili ya mambo ya
kiroho, Mungu ametenga wakat i fulani katika wiki ambao ni wa mafundisho hayo, huku ukiwa pia ni wa mapumziko ya kimwili. Hii inatulete katika amri ya nne IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE. SIKU SITA FANYA KAZI, UTENDE MAMBO YAKO YOTE; LAKINI SIKU YA SABA Nl SABATO YA BWANA MUNGU WAKO. SIKU HIYO
USIFANYE KAZI YEYOTE Wewe,wala mwana wako, …. Maana kwa siku sita, Bwana alizifanya mbingu, nchi, bahari na vyote vilivyomo; akastarehe siku ya saba, kwa hivyo, Bwana
akaibariki siku ya sabato na kuitakasa – Kutoka 20:8-11″.
Hii ndio ile amri ambayo, watu wakitamani kufuata mafundisho ya dunia hii, wameikataa na kufundisha kwamba aina maana. Ukweli ni kwarnba, wakristo wa kweli ambao ndio kanisa la
Mungu bado wanaitunza sabato kama amri ya Mungu na siku ya ibada. Je, kushika sabato kunaonyeshaji upendo wa Mungu? Mtu utafuta nafasi na kuitenga kwa kile kitu ambacho anapenda zaidi, Ikiwa basi tunampenda Mungu kwa mioyo yetu yote, ni lazima tuwe na wakati wa kushinda naye huku tukiongea na kushirikiana. Lakini, ukitaka kukubaliana nami, masumbuko ya
dunia hii yamechukua nafasi ya Mungu katika mioyo yetu. Mungu, hali akielewa hayo, aliitenga siku hii ili atusaidie kupata nafasi ya kushiriki mambo ya kiroho; Eee, tupate nafasi ya kuwasiliana naye kwa maombi na kwa kusoma neno lake.
SABATO ILITENGWA KWA AJILI YA MWANADAMU
Mungu amesema tuikumbuke siku ya sabato – kuonyesha, ilikuweko hata kabla hajaitoa hii amri (soma Kutoka 20:11). Baada ya s i k u sita za uumbajL Mungu alipumzika siku ya saba
(ona Mwa 2:2-3)). Kama vile Mungu aliumba mbingu, nchi, bahar i na vyote vilivyomo ndivyo aliumba sabato pia, Baada ya kumuumba Adamu siku ya sita, ni jambo la kukubalika kuwa,
alishinda naye siku ya sabato akimfundisha sheria na kumuonya dhidi ya shetani.
Amri ya nne inatuambia tuitakase siku ya sabato, Lakini hatu wezi kutakasa kitu ambacho sio kitakatifu, Kwa hivyo, kile Mungu anasema hapa ni;” Tusiharibu utakatifu wa sabato aliouweka hapo, kwa kutenda mapenzi yetu siku hiyo – ona Isaya 58:13.Fikiria! Mungu mwenyewe ndiye aliitenga hii siku kwa utukufu wake, Je, we we mwanadamu u-nani hata ubadili kile Mungu amefanya? soma Isaya 29:16; Zab 94:9-11. Kama vile tuliona awali, Yesu ndiye yule Mungu ambaye aliumba vyote na kunena na wanadamu, Kwa hivyo ndiye aliweka sabato na kuiamrisha.
Hii ndiyo sababu aliwaambia wayahudi;” Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato -Marko 2:28″. Awali, huku akiwafundisha mafarisayo vile sabato inatunzwa, aliwaa mbia: “Sabato iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu (aitunze) lakini mwanadamu hakuumwa kwa ajili ya sabato – Marko 2:27”.
Hapa, Yesu hakusema sabato kwa wayahudi lakini, kwa wanadamu wote – na sio nzito (1 Yohana 5:3). Mafarisayo walikuwa wameongezea rnambo mengi juu ya sabato mpaka
ikawa kama mzigo. Ijapokuwa Yesu aliyaondoa hayo, hii haimaanishi aliwapa watu ruhusa ya kufanya viie wapendavyo siku ya sabato, Hii ni siku ya kusahau shughuli zetu za kila siku na kukusanyika katika ibada, kujifunza mambo ya kiroho.
Mungu anaelewa kuwa sisi wanadamu ni watu wa kusahau haraka. Kwa vile uzima wa milele unategemea kumjua yeye( ona Yohana 17:3), basi aliweka siku ya sabato iwe ukumbusho
kwetu, kuwa yeye ni muumba. Alisema itakuwa ishara kati yake na watu wake milele – ona Kutoka 31:12-17. Wengine watasema ni kwa wa-israeli lakini sivyo, maana imeandikwa – soma
Isaya 56:6-7; Gal6:16.
FURAHIA SABATO YA BWANA
Tunatakiwa kuitunza hii sabato kwa njia gani? Mafarisayo waliongezea mambo yao juu ya; vile inatakiwa, na haitakiwi, hivyo wakafanya sabato kuwa gumu kutunza; Lakini Mungu
hakumaanisha hivyo, Katika Kristo Yesu, alifafanua huku akionyesha maana ya kir oho ya hiyo siku.
JE, UNAPITA MTIHANi WA MUNGU? Wengi ubishana kwamba, sabato iliamrishwa katika agano la kale na kwa hivyo haina maana katika agano jipya. Kweli? Hakuna kitu kilicho mbali na ukweli kushinda hicho maana sabato ilianzishwa pale Edeni, miaka mingi kabla ya agano la kale. Hata kabla hajawapa wa-israeli amri zake pale sinai, alikuwa amewakumbusha sabato (soma Kufoka 16:22-27). Bwana aliwakumbusha hiyo ili awajaribu, aone kama watamtii ona Kutoka 16:4. Anakujaribu sasa hivL Je, utamtii kwa kuitunza sabato yake na hivyo kufaulu katika huu mtihani, ama utaanguka kama waisraeli?
Sabato ndiyo ule mtihani wa Mungu kwa mwanadamu, wa kuonyesha utiivu wake kwa muumba wake; Eee, ya kuonyesha yule atamfuata Bwana kila aendapo, Watu wengi ukubaliana nasi tukiongea mambo kama;” Usiue, usizini, usiibe, usimshuhudie
jirani uongo na usitamani. Lakini yakija mambo ya sabato akili zao huruka. Hii ni kwa sababu, sabato uwatenganisha na karibu watu wote. Je utampenda Mungu arna watu? Sabato imewafanya wengine waachishwe kazi, maana hawawezi kufanya siku hiyo; wengine warnetengwa na jamii zao na ndoa zimevunjika.
Umejikana kiasi hicho ama utaanguka mtihani wa Mungu? Ikiwa utaamua kumfuata, yeye yuko tayari sabato ijayo kuungana nawe katika kukufundisha maisha yake. Mungu anatuambiaje basi kuhusu hii siku ya sabato? u Siku sita fanya kazi utende mambo
yako yote ( Kutoka 20:9). Hii ni sehemu ya hiyo amri ya sabato; Mungu alikusudia tufanye kazi kwa hizi siku sita iii tuwe na mapato. Mithali 19:15. usema ;” Uvivu umtia mtu katika usingizi mzito, na mtu rnvivu ataona njaa”. Yeyote yule ambaye hafanyi kazi siku sita na, yule ambaye anafanya kazi siku ya sabato (saba); Wote wanavunja amri za Mungu.
Basi, hii amri inaendelea kueleza vile kunatakiwa kufanya,” Siku ya sabato , usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako binti yako wala mkazi wako wa kike au kiume ? wala mifugo yako, wala mgeni aliye kwa nyumba yako – Kutoka 20:10″. Kwa hivyo hupaswi kufanya kazi ya aina yoyote siku ya sabato; Kazi yoyote ya kuchokesha.
Mungu hakatai kazi tu peke yake bali, anasema kuwa sabato ni siku ya kukutana kwa ibada – kusanyiko takatifu (ona Walawi 23:2-3). Zaidi ya hii sabato ya wiki, kunazo sabato zingine saba ambazo Mungu ameamrisha kazi isifanywe na kuwe na ibada ( ona Walawi 23:6-37). Hizi ndizo Ezekieli anaongea juu yake – ona Ezek20:12,20. Kwa hivyo sabato ndiyo siku ya kanisa kufanya ibada na kuenda mbele ya Mungu – soma Waebr 12:22-24. Hii ndiyo sababu Mungu alisema; “kama ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato, usifanye anasa yako sik u ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitunza kwa kutozifanya njia zako  mwenyewe ; wala kuyatafuta yakupendezayo; wala kusema
maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana, nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo – Isaya 58:13 -14”. Ili tuweze kutunza sabato kwa njia ya kiroho, ni lazima akili zetu ziwe kwa Mungu na sio kwa mambo ya haya maisha ya kim wili – ya ulimwengu huu. Hivyo basi, tusichukulia sabato karna siku ya kutokufanya kazi yoyote tu bali, kama siku ya kuungana na Mungu katika ibada ya kiroho na kushirikiana na wandugu wenzetu . Ni siku ya maombi na ya kujifunza yanayohusu ufalme ujao wa Mu ngu, huku tukifurahia na kumshukuru Mungu kwa nyimbo kwa yote
anayotutendea.
AMRI YATANO
Muungano wa wanadarnu uanzia kwa, ama umejengwa juu ya msingi wa jamii. Kuthibitisha hiyo, tunaona kwamba, vile jamii zinaendelea kuvunjika ndivyo mataifa yanaendelea kuvunjika pia. Hii imetokana na kutokuweko na heshima juu ya sheria zilindazo,
na kutawala huu ushirikiano.
Mtu mmoja alisema;” Inafaa mtoto afundishwe kuheshirnu wazazi wake kwa maana huu uhusiano, ndio utamsaidia kuelewa vile atahusiana na watu siku za baadaye. Kwa mfano. kutii
wazazi kutamsaidia kujua kutii shulerii, baadaye kutii serikali, na hata mwishowe kumtii Mungu. Sio ajabu basi, Mungu ameiweka hii arnri ya tano katikati, Kwa vile jamii ya kibinadamu ni mfano wa ile ya Mungu, basi rntoto anapofundishwa kuwatii wazazi huwa anatayarishwa kumtii yule mzazi halisi ambaye ni Mungu » baba wetu wa mbinguni . Hii ndiyo sababu Mungu alisema; “WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKOf SIKU ZAKO ZIPATE KUWA NYINGI KATIKA NCHI UPEWAYO NA
BWANA MUNGU WAKO – Kutoka 20:12”. Kutii sheria kwa upande wa wazazi huwa ni kumtii Mungu mwenyewe maana yeye ndiye baba wetu zaidi kuliko huyu wa kibinadamu. Ukiona mtu ambaye hawezi kutii wazazi wake na kuwaheshimu, utakuta kwamba, hawezi kutii Mungu. Kwa mtoto mdogo, mzazi ambaye umlinda, kumlisha na kumfundisha usimama mahali pa Mungu. Kwa hivyo vile atahusiana na huyu mzazi, uonyesha vile atahusiana na Mungu baadaye.
AMRI YENYE AHADI
Katika agano jipya, Paulo alionyesha baraka za kipekee ambazo uambatana na hii amri. Alisema; ” Enyi wat oto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako, maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi- Waefeso 6:1-3″. Hii amri inaongea nasisi wote.Kwa mtoto mdogo, ni kutii kikamillfu, bila kuuliza, Akiendelea kukua,
inampasa mzazi aanze kueleza maana yake. Huu utiivu ni katika Bwana; maana huyu mtoto akikua na kuanza kuelewa ukweli wa Mungu, basi hapo, utiivu utakuwa, kwa Mungu kwanza, halafu kwa mzazi kiasi kile hatamkozesha kwa Mungu (ona Matendo 5:29). Lakini ikiwa amri zao hazipingani na za Mungu, basi inatupasa kuwatii na kuwaheshimu sana Ikiwa mzazi ataheshimiwa, inampasa pia aishi maisha ya heshirna, Maana watoto wakiendelea kukua, inampasa mzazi aanze kuwaelekeza kwa Mungu, kwa kuwafundisha sheria zake; maana imeandikwa;” Nanyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni katika adabu na maonyo ya bwana – Waef 6:4”. Watoto wanapaswa kufundishwa sheria za Mungu kila wakati ( Kumbukumbu 6:7) na kuelekezwa kuwa na imani na upendo mkuu kwake. Amri ya tano inasimamia utiivu kwa mamlaka. Hii ndiyo sababu Paulo aliendelea kufafanua hii amri akisema;
“Kila mtu aitii mamlaka; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu … wapeni wote haki zao, mtu wa kodi; kodi, mtu wa ushuru; ushuru,astahiliye hofu; hofu, astahilioye heshima;
heshima; Waru 13:1-7”. Ni wasi kuwa, kiasi kile mamlaka hayampingi Mungu, basi inatupasa kuitii; maana kwa kuitii,tunamtii Mungu, Kuelewa haya yote uanzia kwa kuwatii wazazi wakati wa utoto. Haya maelezo yote uonyesha ni kwa nini mtoto akiwat ii wazazi ataishi maisha marefu. Mara
nyingi, watoto wale ambao utii wazazi ujiepusha na tabia za kujiharibu – na mwishowe umtii Mungu ata kufikia uzima wa milele – ona Mat 5:5; Ufunuo 5:10).
JE, WATU WAKUBWA WAPASWA KUHESHIMU WAZAZI?
Ijapokuwa watu wakubwa hawapaswi kuzizitiziwa utiivu kwa wazazi, wanapaswa kuwaheshimu sana. Wanapaswa kuwapenda, kuwatunza na kuwaonyesha shukrani kuu kwa sababu waliwalea (ona vile Yesu mwenyewe aliserna kuhusu heshima kwa wazazi – soma Marko7:6-10. Utaona kwamba heshima kwa wazazi inashirikisha kuwasaidia- ona V. 11-13.
Yesu mwenyewe alionyesha mfano kwetu alipokuwa karibu kufa msalabanL Aliangalia chini akiwa pale juu mtini na akaona mama yake Maria akiwa amesimama karibu na Yohana. Halafu
akamwambia mama yake; “mama, tazama, mwanao, Kisha akamwambia Yohana; ” tazama, mama yako .., Yohana l9:26-27”. Yesu alimheshimu mama yake mpaka mwisho; maana, hapa
tunaona akimfanyia mpango wa utunzi kwa yule rnwanafunzi wake aliyempenda sana. Kwa hivyo tuige huu mfano wa Yesu katika kuitii hii amri ya tano.
AMRI YA SITA
Ulimwengu wa leo umejawa na fujo na uuaji. Tunashuhudia watu wasio na hatia wakiuliwa kila siku katika miji; wezi wakiuliwa na polisi, askari wakiuliwa katika vita; tunaona kila siku, watoto ambao hawajazaliwa bado wakiuliwa katika utoaji wa mimba, vijana wanajiuwa; huku mamilioni wakifa kwa magonjwa. Je, umewahi kujiuliza vile Mungu ufikiria juu ya haya mauaji? Ukweli ni kwamba, hana furaha yoyote, na hii ndiyo sababu, kat ika amri yake ya sita alisema, “USIUE” Kutoka 20:13; Kumbukumbu 5:17”.
Hii sheria hairnaanishi kutokuua kila kitu; maana kuna baadhi ya wanyama ambao Mungu alitupatia tuwe tukiua kwa chakula Mungu ndiye mwanzilishi wa maisha; kwa hivyo yeye hafungwi au kuzuiliwa na hii sheria, maana ana uwezo wa kuurnba na kuharibu- soma Ayubu 1:21. Kwa hivyo, nje ya mwanadamu, Mungu alirnpa mtu mamlaka juu ya vingine vyote – ona Mwa 1:28 – 29: 7-2 – ufananishe na 1 Tim 4:3 – 4, Hii haimaanishi kuharibu kama vile tunaona watu wakiuwa faru na ndovu, au kuvyeka misitu kwa ajili ya tamaa ya pesa – ona Mwa 49: 6 – 7 ; Kumbukumbu 22:6-7.
Mungu alimpa rntu mamlaka juu ya mazingira ill ayatunze ( Mwa 2:15), kutunza kunayo tofauti kubwa na kuharibu, Lakini kuua mwanadamu, Mungu alikataza. Katika vitu vyote vya Mungu, mwanadamu peke yake ndiye aliumbwa kwa mfano wa Mungu – ona Mwa 1:26 na ufananishe na 1:25. Mungu sio baba yetu tu kwa kule kutuurnba, bali, zaidi ya kutuumba, kwa njia ya Yesu Kristo anaendelea kuumba tabia yake ndani yetu ili mwishowe atuzae wana wake wa kiroho kama vile yeye alivyo roho 1 Wakor 6:18; Heb 2:10.
Ikiwa basi, tutakuwa washirika wa mau mbile ya utukufu ( 2 Petro 1:4) na kutirnilika katika uungu (Waef 3:19), basi sisi zote tunao nafasi ya kuwa miungu (Yohana 10:34). Maisha ya Mungu
ni ya dhamana kuu, Ijapokuw a sasa tuko katika mwili uharikao, Mungu amekusudia kutushirikisha, kama wana wake, katika hayo maisha yake yasioharibika, Ametupatia haya maisha
ya kimwili ili ndani yake, atupe nafasi ya kujifunza kuishi haya mengine ya kiroho, ill baadaye atupe miili ya kiroho kama ule wake na kutushirikisha katika utukufu wake. Kwa hivyo, kuuwa mtu ni kujaribu kupinga hii nafasi ya masomo ya kiroho ambayo Mungu ametoa kwa wote. Basi, wewe unani upinge na kuzuia kazi ya Mungu? Nani amekupa ruhusa ya kufanya kazi ya Mungu, ambaye peke yake ana haki ya kuua rnaana anaweza kufanya hai? Na sio kuua mtu mwirigine tu, bali na hata kujiua, maana imeandikwa;” Au hamjui kuwa miili yenu ni hekalu …., mliyepewa na Mungu? Ninyi sio mali yenu wenyewe -1Wako6:19”.
KUSUDI LA MUNGU MWANZONI
Katika 2 Wakor 3:7, tutaona ” huduma ya mauti” ambayo Mungu aliwapa wana wa Israeli katika agano la kale Aliwaamuru wawaue wale wanaovunja sheria – Kutoka 21:12-17,23, Hii sio
sawa na vile mtu angeamua kuua, bali ni kama Mungu ameuwa mwenyewe, maan a ndiye ameamrisha Kumbukumbu 7:1-2, Pia kuua pasipo kutarajia, kama kwa njia ya ajali ni tofauti na
kule kuua kutokana na mpango – ona Hesabu 35:9-34.
Hata hivyo, haikuwa kusudi la Mungu hapo mwanzoni, la mwanadamu ajifunze kuua mwanadamu mwenzake . Kwa hi vyo, Mungu katika Kristo Yesu anaumba katika akili za wale
ameita, roho safi ya kupenda, kulinda na kuokoa maisha badala ya ile ya kuharibu na kuua – ona 2 Wakor 3:6.
Akifafanua hii amri ya sita, Yesu alisema “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, ‘Usiue; ….. Bali mimi nawaambieni, kila mtu amwoneaye ndugu yake hasira, itampasa hukumu ….
, Yampasa jehanamu ya moto – Mat 5:21-22.” Yesu hapa anafundisha watu kujiepusha na kile kisababishao kuua – yaani hasira ambayo inazaa chuki. Unaweza kukasirikia mako sa ya mtu, na ukose kumchukia-ona Waefeso 4:26. Hata hivyo, Paulo alionya juu ya kuendelea na hiyo hasira, akisema kuwa, mtu anaweza kumpa shetani nafasi – v 26-27. Kila wakati mtu anaendelea kukasirika, hii inaleta chuki ambayo ndiyo roho ya kuua, Kwa hiv yo, mwenye kuchukia na muuaji ni hali moja. Uzuri ni kutafuta mapatano kati yako na jirani yako – Mat 5:23-24.
Roho wa Mungu utuongoza sisi wakristo kuchunga vitendo na mawazo yetu.Hii ndio sababu maandiko yanasema, ” usilipize ubaya kwa ubaya”. Tenda yali yo mema machoni pa watu wote.
Kiasi kiwezekanacho, tafuta kuwa na amani na watu wote, Msijaribu kulipiza kisasi … maana imeandikwa. ” Kisasi ni juu yangu mimi; nitalipa, asema Bwana – War 12:17-19″.
Mwanadamu katika akili yake ndogo hawezi kujilipiza kwa mwenzake katika haki, kwa hivyo, roho wa Mungu katika Kristo inawa fundisha wakristo kumjua Mungu, na kujua kwamba yeye yuko, na kwamba anawatetea wenye kuonewa, Katika huu ufahamu; Adui yako akiwa na njaa, mlishe, akiwa na kiu mnyweshe, . . . . Waru 12:20- 21”. Hii inakubaliana na yale Yesu alifundisha aliposema; “mpende adui yako, wabariki wakulaanio, watendee wema wakuchukiao, waombee wanaokutumia vibaya – Mat 5:44. Najua wengi wenu wataona hii kuwa jaribu kubwa – yaani kumpenda, kumzaidia na hata kurnwomb ea adui yako. Hii inachukua kuelewa huyu adui kuwa mtu ambaye amedanganyika – ona Luka 23:34.
Ikiwa tutafaulu kuwapenda maadui wetu, ni lazima kwanza tuwachukue karna watu ambao wameumbwa kwa sura ya Mungu, ambao wamedanganywa na shetani, na ambao wakati wao ukifika, Mungu atawafungua macho waone maovu yao. Kuelewa hayo kutatuzaidia kuvumiliana nao huku tukiwasamehe na kuwaornbea ili Mungu awafungue macho, Kuwapuusa na kuwadharahu kwa njia yoyote ile ni kuvunja hii amri ya sita.
UOVU MKUU WA MWANADAMU
Roho ya uuaji ndani ya mwanadamu imejidhihirisha kwa njia ya vita kila mahali; kuanzia kiwango cha jamii hadi kufikia kilele cha kimataifa, Ni kwa nini? Inatoka wapi hii akili mbaya?” Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyo kati yenu yatoka wapi: si, humu katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani wala hamna kitu,Mwaua nakuona wivu, wala
hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana wala hamna kitu kwa kuwa hamuombi. – Yakobo 4:1-2”.
Ni wasi kwamba, uuaji na chuki haviwezi kuisha mpaka akili za w atu zibadilishwe na kufikiria kwa njia tofauti na vile zinafikiria sasa. Hii ndio ile kazi Yesu anafanya kwa njia ya roho
mtakatifu, ambayo huwapa wakristo kufikiria tofauti na walimwengu. Kwa hivyo wakristo wanaendelea kufundishwa njia ya upendo ili, Yesu ajapo, awatumie kufundisha na kuongoza
mataifa yote katika maisha hayo mazuri ambayo matokeo yake ni amani – soma Isaya 2:2-4. Hata hivyo, hii amani imeanza kuonekana kwa wale ambao wako na roho ya Mungu ndani yao.
AMRI YA SABA
Mapenzi ya kimwili nje ya ndoa siku hizi yamekuwa baadhi ya starehe za wanadamu, Kutoka viongozi wa kitaifa adi wale wa kidini, ndiyo, kila mtu anayafanya; walioowa na wenye kuolewa na hata wale ambao hawajaowa ama kuo lewa. Kwa sababu hii, wengi wameanza kuona ndoa kama kitu kisich o na maana, Ni kwa nini Mungu aliianzisha ndoa na kuamrisha watu kufanya
maperizi ya kimwili ndani ya ndoa peke yake?.
Mungu aliweka amri mbili za kulinda ndoa na kuhifadhi uhusiano wa jamii. Ya kwanza ni ile tumeona ya kuwatii na kuwaheshimu wazazL Ya pil i ndio hii ya saba ambayoinasema;-“USIZINI” Kutoka 20:14; Kumbukumbu 5:18.
Baada ya kuonyesha vile maisha ya mwanadamu yalivyo ya dhamana kuu katika amri ya sita, Mungu kwa kupeana amri ya saba, anaendelea kuonyesha ile njia nzuri ya kudumisha
heshima na kuhifadhi huu uhusiano ulio mkubwa zaidi katika rnaisha- maana ndoa na jamii ndio msingi na mwanzo wa maisha mazuri . Kwa sababu hii, amri ya saba inakataza mume aliyeoa
ama rnke aliyeolewa kushirikiana kimapenzi na mtu mwingine isipokuwa mwenzi wake, Ka tika agano la kale, kufanya hivyo kulikuwa kunaletee mtu hukumu ya kifo – ona Walawi 20:10.
Ukweli nl kwamba, kitendo chochote cha zinaa nje ya ndoa; iwe ni kwa mtu aliyeoa ama hajaowa kinavunja amri hii ya saba.
Mungu arneonyesha hicho kitendo kuwa machuk izo mbele yake, na kutoa onyo la uharibifu kwa wote wakifanyao ona Walawi 20:13; Warumi 1:18-32. Kumbuka, ijapokuwa, siku hizi watu wakitenda dhambi hawauliwi wakati huo, agano jipya iriatueleza waziwazi kwamba;” Mshahara wa dhambi ni kifo – Warumi 6:23″ Hivyo basi, hakuna tofauti na agano la kale. Najua wengi ushangaa na kujiuliza;” Kwani kuna ubaya gani kufurahia mapenzi nje ya ndoa?” Kujibu hili swali, ni lazima kwanza tujue maana ya ndoa.
NDOA NI YA NINI. INA MAANA GANI?
Mungu alikuwa na lengo alipoumb a wanadamu – mume na rnke. Kwanza kulingana na ile kusudi la kuzaana na kujaza dunia, Mungu alijua kuwa Adamu pake yake hawezi. Pia katika
uhusiano na upendo wa kijamii, mwanadamu ujifunza mengi kuhusu jamii ya Mungu na maisha yake. Kwa hivyo, Mungu alim uumba mke kutoka kwa ubavu wa mume. Hii ina maana ya
kitu kimoja, kama vile imeandikwa;”…. “Kwa maana hii, mwanaume atamwacha baba yake ni mama yake, na kuambatana na mke nao watakuwa mwili mmoja – Mwa 2:23 – 24”. Wengi udhania kimakosa kuwa rnapenzi ya kimwili ndiyo ule mti uliokatazwa pale Edeni lakini sivyo, Hii ni kwa sababu, Mungu alionyesha Adarnu na Awa wataishi katika ushirikiano wa kimwili kwa njia ya mapenzi soma 1 Wakor 6:16. Huku kushikana kimwili kunaonyesha vile mume na mke wako kitu kimoja hata kwa kila kitu wafanyacho kat ika maisha yaoyote. Kitendo chochote cha mapenzi nje ya ndoa nijitihada la shetani ya kuharibu maana ya huu umoja na kuvunja maisha ya ndoa
ambayo utufunza maisha ya ile jamii kubwa ya Mungu. Hii ndio sababu Paulo alionya akisema;” Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; Kwa maana washerati na wazinzi,
Mungu atawahukurnia adhabu – Waeb 13:4″.
Sababu ingine kubwa ya kusisitizia mapenzi katika ndoa ni kuwezesha watoto wazaliwe na kulelewa katika huo umoja ambao unaleta hali ya ulinzi na upendo kwao; huu ukiwa ni mfano wa vile, katika jamii kubwa ya Mungu yenye umoja na upendo, watu wote wanalindwa na kulishwa. malaki anashuhudia hiyo akisema; ” soma Mal 2:14-15.” Ndoa ndio uhusiano wa kipekee wa kufundisha watu kujitoa kwa wenzao katika maisha ya upendo kama alivyoonyesha Yesu – ona 1Wakor 7: 3-4; Waefeso 5:22-24. Umesikia? Uhusiano wa kijamii katika ndoa unafananishwa na uhusiano wa Kristo na kanisa, Atendaye dhambi ya zinaa huwa ni sawa na yule Mkristo amwachaye Yesu na kuanza kufuata maagizo ya shetani -maana, Paulo akithibitisha uhusiano wa kijamii kuwa somo la vile tutahusiana na Yesu katika jamii ya Mungu, alisema;” kwa sababu hii mume atamwacha baba na mama yake na kuambatana na mke wake ……..” Halafu, hapo akasema;” kuna siri kubwa hapa; lakini naongea kuhusu Kristo na kanisa – Waefeso 5:32-33″. Hii
ndiyo ile sababu kubwa ya shetani kujaribu awezavyo kuharibu ndoa kwa kuongoza watu katika vitendo vya zinaa. Hii ni kwa sababu, maisha na upendo katika jamii yanatufundisha vile
tutaungana na Yesu na Mungu katika jamii ya kiroho . Zinaa inaharibu huu ufahamu na kufanya watu wasielewe maana ya wokovu.
MUNGU UCHUKIA KUVUNJIKA KWA NDOA
Siku hizi, kuvunjika kwa ndoa ni jambo la kawaida, Hii pia inamaanisha kwamba, watu wamekataa kusoma yale masomo tumeona hapo awali yaani –masomo ya vile Mungu katika
Kristo Yesu atatuzaa katika jamii yake na kutushirikisha katika maisha ya upendo wake- ona Wakolo 1:13; Waefeso 3:19,14-15.
Kuonyesha umuhimu wa ndoa, mafarisayo wa lipomjia Yesu wakitaka kujua kama ni halali kuvunja ndoa, Yesu aliwaambia; ” Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo,
aliwaumba mume na mke, na kusema, mtu atamwacha babaye na marnaye, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili rnmoja? Basi sio wawili tena, bali ni mwili mmoja, Kwa hivyo, kile Mungu ameunganisha, mtu asitenganishe- Mat 19:4-6″, Waliposhangaa ni kwa nini Musa aliwaruhusu kutengana , Yesu aliwaambia ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, sio mpango wa Mungu v8-9.
Kuvunja ndoa sio halali kab isa isipokuwa kwa sababu ya zinaa ama, ya mmoja wenu akiwa sio mkristo na angependa kuwacha mwenzake aliye mkristo -ona 1 Wakor 7:15; Mat 19:9.
Mapenzi ya kimwili ndio ile njia ya kipekee Mungu alipanga ya kuwaunganisha ama, kukamilisha upendo kati ya mume na mke. Mapenzi nje ya ndoa uvunja huo muungano na kuharibu ule upendo wa kweli. Hiki ni kitu ambacho Mungu anachukia kabisa – soma Mal 2:14-16. Je, wewe unaichukia?
WACHA KUTAMANI WENGINE ISIPOKUWA MWENZAKO
Mapenzi nje ya ndoa ya mekuwa sehemu ya maisha siku hizi. Elewa jambo hili Kumdanganya mwenzio ni sawa na kuchukua hicho kipawa cha upendo Mungu aiikupa na kukitupa kwa maji. Ijapokuwa unaweza kutubu, kumbuka zile alama utakuwa umeweka kwa akili yako ambazo ni vigumu kuvuta. Eee utakuwa ukikumbuka na hivyo, upendo katika mawazo yako utakuwa umegawanyika. Hii itapunguza ule upendo mngekuwa nao kama
hamngejiuzisha kwa zinaa awali. Kwa ; hivyo kila jamii ya wakristo inatakiwa kujifunza kuungana kimawazo na kimatendo ill waweze kudumisha huu umoja wa mpango wa Mungu.
Hii ndiyo sababu Yesu alifafanua amri ya saba kwa kusema; ”. . . . . Lakini nawaambieni, kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtarnani amekwisha kuzini naye moyoni mwake Mat
5:27-28″ YESU hapa ameonyesha vizuri sana dhambi za zinaa. Maana ikiwa rnawaz o yako yatamweiekea mwingine badala ya mwenzio, hii uanza kulete kutotilia maanani mwenzio na na
uzaa chuki – mwanzo wa kuvunjika kwa ndoa.
Amri za Mungu ni za kutuongoza katika uzuri wote. Mapenzi ya kimwili yaliwekwa na Mungu kama njia ya kuunganisha mume na mke kimawazo na ki-vitendo ili wawe wakamilifu katika
urnoja, Huu muungano ndio shetani anang’ang’ania kuharibu, Uzuri ni kwamba, Yesu amekuja na kutupa roho ya kutuwezesha kumkana huyu shetani ni a kutii amri zote za Mungu ikiwemo hii ya saba, Hii ndi o sababu Paulo anasema; ” yakirnbieni matendo ya zinaa” na tena ” Zikimbieni tamaa za mwili”. – 2 Tim 2:22; Wagal. 5:24.
Mapenzi ya kimwili sio kitu cha kujifurahisha vile mtu  afikiriavyo, bali ni mpango wa Mungu kwa mwanadamu wa kumuelimisha vile maisha ya jamii ya Mungu ni yenye upendo, furaha na umoja.
AMRI YA NANE
Katiba za wanadamu zina mamia ya sheria ambazo zinalinda mali na kuhifadhi vitu vya mtu, Mungu alitoa amri moja tu ambayo inahusisha haya maelezo ya wanadamu yote, na ndiyo hii amri ya
nane ambayo inasema; “USIIBE” – Kutoka 20:15; Kumbukumbu 5:19″. Kutenda kinyume cha hii sheria ni kuiba, Watu ufikiria kuiba ni kuvunja nyumba ya mtu na kuchukua vitu au, kunyang’anya mtu kwa nguvu, Lakini wizi ni mpana. Kwa mfano; kuchukua kalamu offisini bila ruhusa ama hata karatasi ambayo upaswi kuchukua huu ni wizi sawa na ule wa kuiba
pesa. Mungu anaserna; ” .. . Msidanganyike, maana hakuna, msherati …. wala mwizi ambaye wataurithi ufalme wa Mungu – 1 Wakor 6:9-10”. Je, Mungu uchukulia wizi kuwa nini hasa?
Kulingana na amri za Mungu, kuna njia chache sana za kupata na kumiliki kitu, nazo ndizo hizi – (1) Unaweza kupewa kitu, (2) ama ushindeau, (3) unaweza kurithi kutoka kwa mtu, Ikiwa ni
kwa njia ya biashara, utahitaji pesa ambazo ni lazima uwe ulizipata kwa mojawapo ya hizo njia tatu.
Mapato yoyote nje ya hizo njia tatu sana sana huwa ni ya kuiba .
Amri hii ya nane usizitizia umilikaji wa mali. Kwa hivyo vitu haviwezi kuwa vya watu wote, la sivyo wizi haungekuwa wizi. Neno la MUngu inaruhusu biashara – yaani, kuuza na kununua. Hata kuweka pesa kwa benki kwa nia ya kupata riba, ama faida ni halali – ona Luka 19:23; Serikali kutoza ushuru ni sawa pia – ona 1 Samueli 8:10-17.
Hapa kwa kulipa ushuru kwa serikali ndipo raia wengi uvunja amri ya Mungu, maana weng i ujaribu na kukwepa kulipa kodo Watu wengi ujaribu kudanganya serikali kuhusu mapato yao, kitendo ambacho ni kinyume cha neno la Mungu – ona Warumi 13:16-17; ona pia Marko 12:17, Ijapokuwa serikali nyingi uibia raia wake, hii haimaanishi raia nao waibie serikali, maana kisasi ni
juu ya Mungu ona Warumi 12:19.
WIZI KATIKA ULIMWENGU WA BIASHARA.
Wenye viwanda wakati mwingi utengeneza bidhaa za hali ya chini huku wakidanganya ni za hali ya juu na hivyo kuziuza kwa ile bei haifai . Wengine udanganya kwa vipimo ili wapate zaidi ya
vile ingetakiwa. Huu wote ni wizi ambao unavunja amri ya nane ya Mungu – ona Mika 6:11; Mithali 11:1; Amosi 8:4-8.
Tumesikia pia matangazo juu ya uzuri wa bidhaa fulani na hali, zenyewe haziko vi!e wanasema. Kwa njia hii ya uongo, wanav utia wengi na kuwafanya wanunue. Huu pia ni wizi – ona Walawi 19:11.
KUMWIBIA MUNGU
Umewahi kujua kuwa, unaweza kumuibia Mungu? Anasema; ” Je, rntu atamwibia Mungu? lakini watu washangaa; kwa njia gani tunamwibia Mungu? kwa zaka na sadaka – Malaki 3:8″.
Mungu ameagiza watu wote wawe wakirudisha sehemu ya kumi ya mapato yao kwake, na pia sehemu ya mapato yao watoe kama sadaka. Wengi ushangaa! Mungu kweli ana haki ya kudai zaka na sadaka? Hakika; maana wewe na vitu vyote ulivyo navyo ni vyake – Kutoka 19:5; 1 Wakor 6:19 20; Kumbukumbu 8:1, 17-18; Hagai 2:8; . Hata hivyo, ukimtolea fungu la kumi la hiyo mali yake arnekupa, na utoe sadaka kulingana na kile kiwango amekupa, ile imebaki yote ni yako, Amekupa iwe ya matumishi yako.
Eleweni jambo hili. Kabla hujat oa sehemu ya kumi na sadaka, hiyo mali yako huwa bado niya Mungu, umeruhusiwa kuitumia tu baada ya kutoa hiyo sehemu kwa Mungu. Hivi ndivyo wengi wanamwibia Mungu. Usidhanie eti kwa kutoa sehemu ya kumi, unampatia Mungu vitu vyako. Hapana, ni mali ya Mungu . Kwa kumpa, unajiepusha na wizi, maana hii ni mali yake – ona Malaki 3:9-10.
Ni wakati urnetoa hiyo fungu la kumi na sadaka, ambapo matumishi ya mali yako yanakuwa halali. Ummoja wa waizi wa mali ya Mungu?. Kama ndiyo, basi unavunja hii amri ya nane.
Waajiri wengi uwadhulumu wafanyi kazi wao kwa kuwafanyisha kazi ya masaa mengi, huku wakawalipa ujira wa chini kabisa, na pia kuchelewesha hayo malipo. Huu ni wizi pia – ona Walawi 19:13; Yakubu 5:4. Nawe mfanyi kazi, unapolipwa mshahara na huku unategea kazi, unafanya tu wakati umesimamiwa, basi pia wewe unavunja hii amri, maana unamwibia tajiri wako masaa.
MAISHA YA KUTOA
Mwizi akishikwa mara nyingi huwa anafungwa. Lakini huwa hashurutishwi kurudisha mali aliyoiba kwa mwenyewe. Huko jela, anatumia kodi ambayo imelipwa na huyu mwenye maii
aliyoiba. Hivyo huwa ni kama kuzidi kuzorotesha mwenye kuibiwa. Katika amri za Mungu, mwizi anapaswa kurudisha alichoiba – ona Kutoka 22:1, 3-4. Mwenye kudhulumu huwa hapa anazaidiwa. Ikiwa mwizi hawezi kulipa, alikuwa anafany ia huyu aliyemuiba kazi hata itoshane na kile ameiba. Maisha ya Mungu ni ya kutoa, kupeana, na sio kuchukua na kupewa tu. Katika agano jipya, Yesu alisema; kuna baraka, kutoa kuliko kupewa – Acts 20:35”. Kama mtu alikuwa mwizi, haitoshi kuwacha kuiba, ball zaidi ya hiyo, inampasa kufanya kazi hata aweze kuwapa wengine- soma Waefeso 4: 28.
Ni kwa kufanya kazi halali ambapo, tunaweza kupata mali na riziki yetu ya kila siku, Lengo kubwa isiwe ya kutosheleza mahitaii tu ball pia, tuweze kuwa na kitu cha kuwazaidia wenye kuhitaji.
Katika hii sheria ya kiroho, atuibi tu kwa kuchukua vitu vya wenyewe, bali na hata kwa kutokufanya kazi. Mkristo wa kweli ni wa kuwagawanyia wateule kulingana na uwezo wake, na mahitaji yao ona Warumi 12:13 Huku ndiko kujiepusha na, roho na vitendo vya wizi – kutokuvunja amri ya nane.
AMRI YA TISA
Uongo siku hizi umekuwa wa hali ya juu Katika ulimwengu wa biashara, serikalini na hata katika jamii. Watu wakitaka kujionyesha kuwa wenye umaarufu fulani, unena uongo ili wawavutie wateja wao. Eee, uongo siku hizi unachukuliwa kama ujusi wa kimaisha ambapo wenye kudanganya usemekana kuwa werefu. Ukweli ni kwarnba, uongo uvunja jamii na hata uma kwa
jumla. Tena, uongo haujengi maana, adanganyaye ufanya hivyo kwa kukataa kutenda yampasayo. Mungu akijua uharibifu uletwao na uongo, alitoa hii amri ya tisa akasema;
USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO Kutoka 20:16
Wengi katika mahakama uitwa kama mashahidi katika kesi huku wakielewa vizuri sana kwamba, yale wanayoshuhudia ni ya uongo, wanachagua kud umisha urafiki kwa wenzao huku
wakivunja amri za Mungu – ona Luka 16:15; Malawi 19:11. Uongo ni mpana maana utakuta kwamba; masengenyo, kueneza ufumi, kuiba, kujikweza- haya yote ni ya uongo. Maandiko
yanasema; ” Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu kuwa shahidi wa udhalimu Kutoka 23:1-2″. Utakuta kwamba, wizi wa vifaa ni rahisi maana hivi ni vitu mtu
anaweza kurudisha. Lakini wizi wa kuharibia mtu jina ama tabia, kwa kumshuhudia mambo ya uongo haiwezi kurudishwa. Mtu wa kuharibu ma jina ya wengine anafananishwa na silaha hatari,
maana juu yake imeandikwa; “Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo ni nyundo, ni panga, na mshale hatari – Mith. 25:18”. Kwa kweli, mwenye kumshuhudia jirani uongo ni sawa na
muuwaji,.
Mungu uchukia shahidi wa uonqo – ona Mith 6:19. Kwa hivyo, kueneza uvumi ama kuwa shahidi wa jarnbo lisilo la kweli ni dhambi kubwa, Ni kwa njia ya ushuhuda wa uo ngo ambapo Yesu aliuwawa maana imeandikwa; “Kwa maana wengi walimshuhudia uongo lakini ushuhuda wao haukupatana – Marko 14:56″. Mungu aishie milele na arnbaye arnetuita kwa kanisa lake lililo katika Kristo Yesu ametuamrisha kuongea ukweli kila wakati.
Anasema hivi; “ Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; bali, shahidi wa uongo utamka hila … mdomo wa kweli utaimarishwa hata milele bali, ulimi wa uongo ni wa muda tu … Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; bali, watendao uaminifu ni furaha yake – Mith 12:17,19, 22″.
Hii haimaanishi eti mtu aseme mambo yote ayajuayo maana, rnaandiko yanazidi kusema; ” Kwa sababu hii, inatu pasa kuwa waangalifu tunapotoa habari yoyote; Eee, tunapaswa kuwa
wenye hekima katika matamshi yetu yote, yawe ni ya kweli. Hakuna njia nyingine ambayo mwanadamu anaweza kuhusiana kikamilifu na Mungu isipokuwa ile ya kunena, na kudumu katika
kweli maana;’ Mungu ni kweli ona Kumbukumbu 32:4; Zab 31″5; Isaya 65:16″. Soma pia Yohana 14:6; Zab  119:142,151,160; Yohana 17:17.
Agano la kale linasema kuwa, Mungu si mwanadamu hata aongee uongo -Hesabu 23:19; Samueli 15:29; Trto 1:2; Heb 6:18. Inatupasa tuelewe haya mafungu vizuri maana, tusipoyaelewa,
hatutaweza kuwa na ujasiri wa kutegemea na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kuthibitisha hayo, maandiko yanasema; ” Bwana yu karibu na wote wamwitao; wote wamwitao kwa uaminifu
– Zab 145:1-18″. Kwa hivyo, pasipo kule kuishi kulingana na neno la Mungu ambayo ndiyo kweli, waongo na hivyo, hatutaweza kumwabudu, maana imeandikwa;” Mungu ni roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli – Yohana 4: 24 ; ona pia 2 Yohana 4.
UKWELI AMA ADHABU
Shahidi wa uongo hataepuka adhabu, wala hataokoka … ataangamia – Mith 19:5, 9″ ona pia Kumbukumbu 19:16-21; Warumi 6:23. Ukweli ndio utadumu hata milele. Akishuhudia hiyo kuhusu ufalme wa Mungu katika ulimwengu wa kesho , Zekaria alisema; “……. na Yerusalemu mji wa kweli – Zek 8:3”. ona pia Ufu 21:27. Ni dhairi kwamba waongo hawatauingia
kamwe huo mji maana ni mji wa kweli – ona Ufu 22:15; 21:8, Uriaona vile uongo ni mbaya? Ikiwa tutatii hii amri ya Mungu, ni lazima tujitahidi kujiepusha na uongo wa kila aina, Ni lazima
tumgeukie Mungu kwa mioyo yetu yote, huku tukimlilia atusamehe na kutuongoza katika kweli; la sivyo tutaangamia.
Wale wagunduao maovu ya dunia hii ujitenga na mambo yake na kujiunga na Mungu, Yeremia alikuwa mmoja wao. Sikia vile alise ma; “ Laiti ningekuwa na mahali pa kuka jangwani, kibanda cha wasafiri, nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.
Huupinda ulimi wao kama upinde, ill kusema uongo;
nao wamepata nguvu katika nchi; lakini sio katika uaminifu, maana uendelea toka ubaya adi ubaya, wala hawanijui mimi, asema Bwana. Jihadharini kila mtu na jirani yake, wala msitumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongoa, na kila jirani atakwenda huku na huko na kuzingizia.
Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema  ukweli, Wameuzoeza ulimi wao kusema uongo’ hujidhohofisha ili kutenda uovu … Yer 9:2-6”. Hali tukielewa hayo, ya kwamba ulimwengu huu umetawaliwa na shetani ambaye ni baba wa uongo, inatupasa kujie pusha na maisha yake na kukaa katika kweli. Hii ni kwa sababu, Mungu anaonya kuhusu huu ulimwengu na maisha yake akisema;” Kwa maana gadhabu ya
Mungu imedhihirishwa kutoka rnbinguni, juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu – Warurni 1:18″. Ona pia fungu la 25. Utachagua nini rafiki yangu? Kuangamia na
uongo ama kudumu katika ukweli?
MWANZO NA MWISHO WA UONGO
Shetani ndiye mwanzilishi wa uongo. Uongo ni kitu chochote kisemwacho, kufanywa au kufikiriwa nje ya neno la Mungu. Yale yote wa nasayansi na wanatekinologia wanafundisha na
kuongoza watu kufanya kinyume cha neno la Mungu ni ya shetani na ni uongo – ona Warumi 1:23-25; Yohana 8:44. Kama mfalme wa duriia hii, shetani amefaulu kudanganya karibu dunia
yote – ona Ufu 12:9; Waefe 2:2; Yeremia 17:9, Hata hivyo, Mungu katika Kristo Yesu amefungua njia ill, wote watakaopewa kuielewa waanze kuyaacha maisha ya uongo na kuanza kuishi katika kweli ona Wakolo 3:9; Waefe 4:15-25. Kuongea ukweli peke yake hakutoshi kuleta ukamilifu. Inatupasa kuishi kwa kutii na kuitenda hiyo kweli. Ona vile Daudi aligundua kuhusu uu
ukweli Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni … Zab 51:6”. Hii ni kusema; ikiwa mtu ataongea ukweli kwa halali, ni lazirna moyo, mawazo, na fikira zake ziwe zimejawa na huo
ukweli; La sivyo, atakuwa mnafiki. Kumbuka, Mungu ambaye ndiye hakimu, anaona ndani ya moyo wako, na ndiye unasimama mbele yake. : Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri
zake, ni muongo wala kweli haimo ndani yake 1 Yohana 2:4”. Kushika hapa kuna maanisha, kuishi kulingana na hizo amri,
Hebu fikiria ulimwengu usio na uongo wa aina yoyote He! jaribu kufikiria vile ingekuwa kama kila mtu angeongea ukweli. Hakungekuwa na wizi, uesherati, ushuhuda wa uongo, n.k, Yesu
Kristo alihubiri juu ya kuja kwa ufalme wa Mungu, ambao juu yake, Petro alisema;” Lakini kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya; ambayo, haki yakaa ndani yake – 2
Petro 3:13”. Ufalme huu ndio utamaliza uongo kabisa. Hata hivyo, Mungu ameita wachachewakati huu ambao kwa njia ya Yesu Kristo, ameanza kuwafundisha kukataa uongo na kuishi katika kweli.
Hawa ndio wanaitwa ” Kanisa la Mungu” na ndio wanakuletea huu ukweli katika vipindi vya “ULIMWENGU WA KESHO”, yaani – ufalme wa Mungu. Je, unaielewa hii sauti? Heri wewe ikiwa utaitii.
AMRI YA KUMI
Kwa kuwa tamaa, yaani – kutaka cha rnwenzio ni kupana, Mungu amekutaja katika amri ya mwisho. Ni kupana kwa sababu kunashughulika na ile wazo ambayo inavunja zile amri zingine zote – yaani nia ya ubinafsi ambayo haiwezi kutii mwingine, Sio kwamba eti, hii nia ya ubinafsi inataka kupata vitu vyote tu, bali, inazaa hata nia za wizi, uesherati n.k., ambazo ni kinyume cha Mungu na wanadamu pia. Mungu akielewa hayo, alimalizia amri zake kwa kusema, “USITAMANI NYUMBA YA MWENZIO, WALA BIBI YAKE, WALA MJAKAZI WAKE AU CHOCHOTE KILE CHA MWENZAKO – Kutoka 20:17; Kumbukumbu 5:21”.
Umeona uzito wa hiyo amri? Hii sheria inahusiana na jirani – mwanadamu mwenzako Hii amri ya mwisho inashughulikia sana mawazo na nia za moyo ona Warumi 7:7,14. Tamaa ni chanzo cha aina nyingi za dhambi. Paulo akishuhudia hayo alisema; u Dhambi ikijipatia nafasi kupitia kwa amri, iliniletea kila aina ya tamaa mbaya- War 7:8″. Wengi wanaweza kushangaa vile
anavutwa na tamaa zake. Tamaa inapokornaa uzaa dhambi- Yakubu 1:14-15′ Ona pia Warumi 1:28-32; Waef 5: 3-7; WakoIo3:5-7. Maandiko yanaendelea kusema kwamba; “Yeyote
achukiaye tamaa mbaya ataona maisha marefu – Mith 28:16”. Hii ni kweli maana hawezi kuhatarisha rnaisha huku akitaka zaidi na zaidi.
TAMAA, UMILIKAJI, CHEO
Wengi watafikiria juu ya vile vitu vimetajwa katika hii amri ambavyo hatupaswi kutamani Lakini ukiangalia maneno ya mwisho yanasema; “….. na kila kitu alicho nacho jirani yako”. Kila kitu hapa kinaonyesha vyote. Hufai kutamani kazi ya mwenzio, au mamlaka yake, ama kujari bu kuchukua sifa ya mwingine, Hii imejumulishwa kwa haya maneno” ….. tamaa za mwili, tamaa za macho na kiburi cha maisha – 1 Yohana 2:16”.
Tamaa za mwili zinahusiana na mali, na matakwa ya kimwili ya njaa, usinzi, ulevi na nia yoyote ile ya kimwili. Neno la Mungu inaonya kwamba; “… wasio waaminifu watatengwa na
tamaa zao – Mith 11:6”. Paulo anasema; “ basi na tuenende katika haki … sio kwa wivu, tamaa na ugomvi; bali , jitieni katika bwana msizitimize tamaa za mwili -Warumi 13:13 -14″. ona
Warumi 6:12.
Wengi ujaribu kutimiza tamaa zao kwa kupigana. Hii inazaa vita. Vita nyingi na ugomvi utokana na tamaa za mwili, huku watu wakijaribu kupata zaidi katika mali, mamlaka n.k. ona Yakubu 4:1-2; Mika 2:2. Hii tamaa ya mwili uzaliwa na tamaa ya macho – ona Mith 27:20; 1Timo 6:6-10. Yesu alionya: ‘ Jihadharini na tamaa, maana maisha ya mtu hayategemei vitu alivyonavyo- Luka 12:15″.Tukianza kutamani mali na vitu vya kimwili, ile lengo la maisha inatupotelea. Daudi akielewa hayo aliomba hivi ” Dumisha akili yang u kwa ushuhuda wako na sio kwa tamaa. Yageuze macho yangu yasiangalie vitu visio na maana. Nihuishe katika njia zako –Zab 119:36-37”.
Wengine utafuta utajiri kwa kule kuwa na mati nyingi na hii inaingia katika kiburi cha maisha ambacho pia ni aina ya tarna a mbaya – Eee, kutaka uvumi, mamlaka n,k, utaona hii ikifanya
wanasiasa kuhaibishana kwa matuzi na kupigana huku wakitafuta uongozi – Kiburi cha maisha.
Mungu anawaambia; f Kukwezwa hakutoki mashariki wala rnagharibi wala kuzini. Ba li, MUngu ndiye hakimu. Yeye umkweza mmoja na kumteresha mwingine Zab 75:6 “.
HIZI AMRI ZINAUNGANA
Chochote kile mwanadamu ameruhusu kiingia kati yake na Mungu ni sanamu na hivyo ni Mungu mwingine. Kwa hivyo hii amri ya mwisho inaungana na ya kwanza na ya pili kwa njia hii;”
. ta m a a ni ibada ya sanamu- Wakolo3:5” , na” . . . . atamaniye ni mwabudu sanamu Waef 5:5”.
Ukianza kutamani vitu zaidiya kumwabudu Mungu, hivyo vinakuwa sanarnu ambazo unaziabudu – ona Warumi 6:16. Kwa njia hii unakosa wakati wakusoma neno la Mungu ama
kumwomba. Hiiinakufanya utegemee hivi vitu badala ya Mungu muumba wako, hivyo, vinakuwa Mungu wako – ona Mark 4:19.
Ni lazima rnkristo wa kweli amuweke Mungu na ufalme wake mbele ya vitu vyote – ona Mat 6:33, Ni lazima ajifunze kutosheka na kile ako nacho – Waebr 13: 5; Mhubiri 6:9, Inampasa mkristo ajivunze kumtegemea Mungu na sio mali – 1 Tim 6:17-19. Eee inatupasa tujivunze kutoa vile Mungu atoavyo- Matendo 20:35. Ni kwa kujivunza kutumikia wanadamu wenzetu, na kumwabudu Mungu muumba wetu ambapo, tutapata furah a na utimilifu katika maisha haya na, katika ulimwengu wa kesho, Mungu atatupa urithi wa vitu vyote, na uzima wa milele.
AMRI MPYA
Kama vile tumeona katika kitabu, Yesu hakuziondoa wala kuzibadili amri za Mungu , bali alizitenda na kuzifafanua Hii ni kwa s ababu, mbali na kuzitenda, alionyesha vile imetupasa
kuzishika hata katika mawazo yetu. Kumbuka jiibu ia Yesu kwa yule kijana ambaye alitaka kujua namna ya kurithi ufalme – soma Mat 19:16 -17 Kwa hivyo, njia ya wokovu ni kuzitii amri za Mungu ambako ndiko kutenda mapenzi yake – ona, Mat 7:21.
Kwa vile Yesu alituonyesha njia ya uzima, na chochote kile alitenda kilikuwa ni kielelezo (Yohana 13:14; 1 Petro 2:21) Kwetu, basi imetupasa kuzit ii amri za Mungu, maana yeye alizitii – soma Yohana 15:10; 8: 28 -29. Alipowatuma mitume baada ya kufufuka (Mat 28:18-19), ill waihubiri inji!i duniani kote, aliwaambia wawafundishe waaminio, yale yote aliyowaamuru. Yesu aliwaamuruje?” Mkinipenda, mtazishika amri zangu … Yohan 14:15”. Tena aliwaambia;” Maneno niwaambiao si yangu, bali ni yake yeye (baba) aliyenituma ~ Yohana 7:16; 12:49, Ni jambo lililo dhairi kwamba, mafundisho ya injili ya Yesu ni juu ya Mungu, ufalme wake na amri zake ambazo ndizo maisha ya huo ufalme. Lakini hii amri rnpya ya Yesu ni gani?.
MPENDANE NINYI KWA NINYI
Ni mahali pamoja tu katika biblia ambapo Yesu aliongea kuhusu amri mpya Alisema, ” …. mpendane kama alivyowapenda … Yohana 13:34 – 35″.Kile mtume Yohana alieleza baadaye ni hiki hiki ambacho Yesu alisema. Katika agano la kale, Mungu aliwaambia,”mpende jirani yako vile ujipendavyo
mwenyewe”, Lakini Yesu alisema , ” … kama nalivyowapenda”, yesu alitupendaje? Yohana 10:11;15:13. Zaidi ya vile ajipendavyo maana alikufa kwa ajili yetu. Pia alionyesha kwa vitendo maana ya amri zake. Huu ndio up endo wa Mungu uletwao na kuzishika amri zake. Hii ndiyo maana ya amri mpya (ona pia 1 Yohana 3:16). Kwa hivyo sio eti ni amri nyingine mbali ni undani wa zile zile kumi -ona Warumi 13:10.
Eee Yesu hakuwa na miungu mingine isipokuwa yule mmoia alive mtuma na ambaye ndiye muumba na wa kweli – ona Yohana 7:16-17; 8:29;5:19-20. Amewaachia wakristo wa kweli
kielelezo ill wafuate nyayo zake. Yesu alijikabidhi kikamilifu kwa Mungu akawa chombo chake cha kufanyia kazi – ona Yohana 5:30. Wewe huko kama yeye? Maandik o yanasema;” Yeye asemaye anamjua imempasa kuenenda sawa na vile alienenda – 1 Yohana 2:6”. Mitume walijikabidhi vivyo hivyo maana walifuata nyayo zake.
Sikia vile mmoja wao alisema ” Nimesulubiwa pamoja na Kristo waia sio mimi niishio bali Yesu aishiye ndani yangu – Waga l2:20 Na wewe je? Kwa vile Yesu abadiliki (Waebr 13:8) na ni yeye anaishi (Kwa n j i a ya roho (mtakatifu) ndani ya wakristo, basi ataendelea kutii amri za Mungu. Hii ndiyo sababu, wateule ni wale ” wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu – Ufunuo 14:12; 2:17.
UJUMBE WA TANGU MWANZO
Yule mtume ambaye Yesu alimpenda zaidi alinena hivi;” Wandugu siwaandikii amri mpya bali, amri ya kale ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Hili amri ya zamani ni ile neno mmesikia tangu mwanzo, Tena, nawaandikia amri mpya, ambayo ni kweli ndani yake, na ndani yenu, maana giza inaendelea kupita, na nuru ya kweli inaangaza . Yeye asemaye yuko katika nuru na anamchukia ndugu yake, yuko gizani hata sasa – 1 Yohana 2:7-9”.
Kwa hivyo, walikuwa na neno hili tangu mwanzo. Mwanzo gani? “Maana huu ndio ujumbe mliopata tangu mwanzo,’ Kwamba tupendane, na sio kama Kaini ambaye akijawa na yule mwovu, alimuua nduguye – Yohana 3:11-12;” ona pia Yohana 1:1-2. Kwa hivyo, hili neno ni lile la tangu kuumbwa kwa dunia maana Mungu abadiliki; ona Malaki 3:6; Mhubiri 3:14.
Utaona kwamba, hakuna upendo mwingine katika biblia na  katika dunia yote, isipokuwa ule unaelezwa na neno la Mungu. Chochote kinachotajwa katika agano jipya kinatilia mkazo na
nguvu, kile cha agano la kale. Amri kumi za Mungu ndizo njia ile ambayo upendo unapitia, Eee, zinaeleza kule kupenda haza. Mungu atatuzaa katika jamii yake na kutupa urithi wa milele katika ufalme wake, kabla hajafanya hivyo, hivi sasa anaendelea kuumba akili yake ndani yetu. Amri zake ndizo hiyo akili yake ambayo ni lazima iumbike ndani yetu kabla hajatupa uzima wa milele. Kwa kule kuzitafakari mchana na usiku (Kumbukumbu 6:6-9; Zaburi 1:2),
Mungu ndani ya Yesu Kristo, na kwa njia ya roho mtakatifu, anaendelea kuziandika hizi amri ndani ya mioyo yetu maana ndizo zitakuwa maisha ya wale watakaofaulu kuingia na kuriithi huo ufalme wake. Hii ndiyo maana ya agano jipya – Soma Yeremia 31:33; Ezekieli 36:27; Warumi 8:4.
Ndugu, unataka kuwa Mkristo wa kweli? “zishike amri za Mungu – Mat 19:17”.