KHOFH

Pentecosti 2007

na Bill Goff

Tuko hapa wandugu, kwenye mwisho wa sikukuu za mwaka, ambazo zimetulete kwa sikukuu yetu “sikukuu ya pentekosti”.kwa mara nyingine tena, tunazo sabato zinazofuatana na, leo ikiwa ni siku ya hamsini.

Siku ya 49 ni siku muhimu sana kwetu kwani inaonyesha; “kumalizika kwa mjengo wa kanisa la Mungu”

Pentekosti ni sikukuu ya ajabu yenye majina tofauti, yaani – pentekosti, sikukuu ya majuma, sikukuu ya malimbuko n.k.

Mwaka huu Mungu amezipanga sikukuu za kwanza kwa njia ya ajabu, yaani

kuanza na sabato za kufuatana na pia kumaliza nazo.

Muumba wetu anataka tuangalie sana siku yetu, siku ya mwisho. Hapa kunao

mifano mingi. Kunayo sababu Muumba wetu anataka tutazame sana siku ya

mwisho.

Tuliona viile sikukuu ya mikate isiyochachwa inatufundisha kuwacha dhambi.

Tuliona vile inatufundisha kutoa dhambi na kuvaa utakatifu. Hii ndiyo maana ya hii

hesabu yote, ikiangazia katika sikukuu ya mikate isiyochachwa, yaani mwanzo wa

kutoa roho mbaya na kuvaa roho njema ya uhaki.

Kumbuka, siku ya 50 ni siku ile, ambayo ile migando miwili inatikizwa mbele za

Mungu ili kukubaliwa naye. Leo naamini, tutaweza kuelewa, kile Muumba mbingu

na nchi ana- tufundisha kupitia kwa hii migando miwili. Eee, kile anataka tuelewe.

Kile tutaongea hapa siku hii ya Pentekosti hakihusu tu kanisa mbali, wanadamu

wote wanaoishi duniani leo.

Sikukuu ya pentekosti ni sikukuu ya wazaliwa wa kwanza wale watakaoshiriki

ufufuo wa kwanza.

Tunaelekea wakati ambao, serikali zilioko sasa, na mamlaka yake yote

yataondolewa na badla yake kuje Ufalme wa Mungu.

Eee, SERIKALI YA UFALME WA MUNGU.

Tunaelekea wakati ambapo, uongo, na uovu wa kila aina utaondolewa, na Yesu

pamoja na Wateule wachukue nafasi zao, na kutawala kwa miaka elfu moja.

Tunaishi wakati wa mwisho wa huu ulimwengu. Huu ndio ule wakati ambao Yesu

alituonya juu yake.

Tunaishi huo wakati ambao matukio ya kila aina na ambayo hayaeleweki

yanatokea. Dunia haitaisha lakini ulimwengu, ndio, haya maisha ya wakati huu

yatapita, yatakwisha. Hapa tunajadili matukio ya wakati huu wa mwisho. Inahusu

matayarisho ya wale watakao- tawala pamoja na Kristo na matayarisho ya afisi

zao.

Wandugu, wakati wa kutuzwa kwa wale watakaofaulu umekaribia.

Hebu tusome Yohana 18:36.

Hapa, Yesu aliletwa mbele ya Pilato, ambako aliulizwa, “Wewe ni Mfalme wa

Wayahudi?”. Yesu hakukataa kwamba yeye ni mfalme. Alimwambia Pilato

kwamba, nikwasababu hiyo alizaliwa.

Yohana 18:36 – Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ungelikuwa wa

ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania – – .

Yesu alionyesha waziwazi kuwa ufalme wake sio wa wakati huo, na hata sasa

hauko bado. Kwanza, wengi wa wale watakaoutawala bado wako makaburini,

kama Ibrahimu na Mfalme Daudi.

Tuende Mathayo 19:28. kuna kitu muhimu hapa.

Hapa, Yesu aliwaambia wanafunzi kwamba, watakaa juu ya viti vya enzi na

kuhukumu. Cha muhimu hapa ni; “hii itakuwa lini?” MAT. 19:28.

“Amini amini nawaambieni. Ninyi mulioambatana nami, wakati mwana wa Adamu

atakaa kwenye kiti cha enze cha utukufu wake, ninyi pia mtakaa kwenye viti vya

nezi na kuwahukumu – -.”

Hii inadhibitisha vizuri sana kwamba, ni wakati ujao na sio sasa. Ni wakati Yesu

atakapokuja (ona Matendo 3:21).

Wandugu, hatuishi wakati ambao Yesu anaanza ujenzi bali, wakati ambao

anaendelea kumalizia.

Tuende katika,Isa 9:7.

Tuanze fungu la 6.

Maana kwetu mtoto amezaliwa, mtoto wa kiume, na ufalme utakuwa mabegani

mwake. Naye ataitwa Mshauri wa ajabu, Mungu Mkuu, Baba wa milele, Mfalme wa

Amani.

Mungu wetu ni wa mipango. Kile anachofanya sasa ni mpango aliouweka tangu

mwanzo ambao anautekeleza sasa.

Ufalme wa Mungu ukaribu kuimarishwa katika dunia hii.

Yesu atatawala pamoja na wateule kwa miaka elfu moja. ( ona 1 Wathe.3:13;

Yuda 1:14).

Hawa wateule si wengine ila wale manabii na mitume na, wale wa kanisa ambao

watahitimu katika utakatifu. (ona Ufunuo.19:11).

Ufunuo 19:11, 12-13

12: macho yake ni kama miali ya moto. Na katika kichwa chake, kuna taji nyingi

13: na jina lake anaitwa NENO LA MUNGU

14: na majeshi wa mbinguni yataambatana naye.

Yesu atashuka kutoka mbinguni na malaika wake. Na wateule watakutana naye

mawinguni alafu washuke pamoja..

Kila wakati tunasoma 1 Wakorintho. 15:52:

Ghafla, kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho. Maana

parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na kuharibika . na sisi

tutabadilishwa.

Huu ndio wakati Yesu atawafufua wafu na kuwabadilisha wale walio hai na walio

katika imani.

Soma hesabu.10:1-4:

Tunaongea kuhusu wateule wa Mungu hapa, wale ambao watafufuliwa na

kuimarishwa siku ya mwisho. ( ona Ufu.19:14-16).

Ufunuo 19:19: nikaona ule mnyama na wafalme wa dunia na majeshi yao

wamekusanyika ili kufanya vita na yule aipandayo ile farasi, na majeshi yake.

Jeshi lake linahusu wale waliovalishwa katani nyeupe.- – – katani nyeupe ni

matendo ya haki ya wateule. Wale walioshinda na kuumbika utakatifu.

Jee, tutakuwa baadhi yao? Eee, tutamlaki Yesu mawinguni na kurudi naye?

HUU NDIO WITO WETU! NI UAMUZI WETU PIA!

Tunahitaji kuchagua kwa hekima. Hebu tusome Luka.14:15.

Tunaishi wakati wa mwisho, wakati ambao ufalme wa Mungu hauko katika akili za

wengi.

Leo, watu wanashughulikia mambo mengine. Mambo ambayo yanahusu haya

maisha ya kimwili badala ya kujihusisha na matayarisho ya ufalme wa Mungu

unaokuja.

Luka.14:15-17. inazungunzia kuhusu karamu ambayo wale watakaoshinda

watahudhuria. Sasa hivi, kupitia kwa huu ujumbe, Yesu anatuita sisi Wakristo kwa

hiyo karamu (onaLuka.14:17).

Tunaharibu wakati mwingi tukizungumzia makosa ya wengine, na kundanganyika

huku tukisahau kujitayarisha sisi wenyewe. Huu ni wakati wa kila mtu kujiangalia

yeye mwenyewe.

V.18-19- vinaonyesha vile tunaweza kujipa sababu za kutomfuata Yesu hata

kukataa huu wito na hivyo, tukakosa kuhudhuria hiyo karamu.

Wengi wameitwa lakini, wachache watachaguliwa. Hii ni kwa sababu wengini

wamejihusisha na masumbuko ya maisha haya. (ona V.24).

Lakini, nawaambieni, dhamana ya maisha ya kimwili haifai mtu kuibadilisha na

haya maisha ya utukufu ambayo Mungu ametuitia.

Hebu tusimame hapa kidogo na tujiulize. Huu ulimwengu wa sasa ulitoka wapi?

Ulianzishwa na nani?

Sisi tumezaliwa juzi wakati maisha yameenda hatua kubwa tangu yaanze.

Tumeingilia katikati. Kwa hivyo, ikiwa tutaelewa chanzo, ni lazima tumuulize

Mungu.

Tunaishi katika ulimweng u na ufalme ulio tofauti na ule wa Mungu tunaongojea.

Huu ulimwengu tunaoishi leo ulianza miaka mingi iliyopita wakati wa uasi wa

malaika chini ya uongozi wa Lusifa ambaye ndiye anaitwa shetani leo.

Mipango, matendo, fikira na nia za mioyo ya huu ulimwengu zilianzishwa na

shetani, na ndizo leo tunaita Babeli.

Yameendelea kupita falme nyingi tofauti hata kufikia sasa. Hata hivyo ni yale yale.

Mungu wetu ambaye anajua mwisho kutoka mwanzo anataka pia tujue kama yeye.

(Soma Dan.2:1-45).

Utaona vile haya maisha yameendela kupitia falme moja hadi nyingine.

Pia utaona vile kuja kwa ufalme wa Mungu kumekaribia sana. (v.44)

Dan.7:24-5 inaongea juu ya falme kumi zitakazotokea duniani.

Sehemu ya huu unabii imetokea na sehemu nyingine iko bado lakini iko karibu

sana.

Dan.2:42-45 inaonyesha vizuri sana ule wakati ambao yesu ataimarisha ufalme

wake hapa duniani.

Matunda ya maisha ya ulimwengu huu ni uovu onaouona sasa. Na kama Mungu

hataingilia, ulimwengu utajimaliza, lakini ataingilia.

(Soma Isa.3:10).

Hii ndiyo sababu Mungu anatuita sisi wakanisa lake akisema “TOKENI KATI YAKE

ENYI WATU WANGU.”

Kile Mungu alifanya wakati wa Nuhu kabla ya gharika, ndicho anafanya kupia kwa

kanisa lake leo kabla ya ile sikukuu ya Bwana.

Mungu anatuonaje wandugu? Kama Nuhu au kama walimwengu wa wakati wake

(soma Mwa.7:1)?

Gadhabu ya Mungu itaujia ulimwengu wa sasa ghafula vile iliujia ulimwengu wa

Nuhu, pasipo matarajio ya wengi.

Onyo inaendelea sasa vile iliendelea wakati huo kabla ya gharika.

Unaisikia? Unaielewa? Kama ndiyo, unafanya nini na huo ufahamu?

Huu ni wakati wa kanisa kumkaribia Mungu kuliko wakati wowote ule.

Ni wakati wa kuishi kufuatia kila agizo la mungu, ili tuweze kuumbika hayo maisha

yake.

Kanisa linaishi wakati wa Leodikia, kipindi chake cha mwisho.

Kristo anaita mara ya mwisho huku akionya kuwatema chini wale ambao

hawataisikia sauti yake na kuitii (soma 1 Petro.3:14).

Wakati umefika wa kujitoa kabisa na kujitenga na mienendo ya ulimwengu huuona

2Tim.2:4

Tunaongea mambo ya kuhesabu hapa. Hesabu gharama, kama umeamua

kuyaacha yote ya ulimengu huu, ili uweze kuyapokea yote ya ufalme wa Mungu.

Walawi.23:15 inaongea juu ya kanisa, vile imechukuliwa mimba na inaongojea

kuzaliwa. Lazima tukamilishwe hata ajapo Yesu, tukutwe bila mawaa yeyote

(Ufu.3:21).

Lakini tukumbuke kitu muhimu hapa./ kwa uwezo wetu wenywe, hatuwezi. Kwa

hivyo, inatupasa tumwombe Mungu kwa kila jambo ili atupe uwezo, maana yeye

ndiye anayetujenga, sisi ni mjengo wake.

Lazima akija Yesu, tuwe tumekamilishwa, tayari kwa utawala katika ufalme wa

Mungu (1Wafalme.7:6).

Tunapaswa pia kuwa watu wa kutafuta sana ukweli wa kila jambo kwa kusoma

maandiko ili tuhakikishe tunatenda mapenzi yake.

Tukifanya hayo, basi, wakati wa dhiki kuu utakapokuja, yeye Mungu atatulinda na

kutuongoza hata atuingize katika ufalme wake.

Watu wengi hutafuta kuimarika kimwili. Tunatafuta kuimarika kiroho. Tunapotunza hii sikukuu ya Pentekosti, hebu tukumbuke hayo yote.

Tutajitayarisha? Kila mtu ajijibu.