KHOFH

KANISA NI NINI? 

 Hakikisha uko na biblia yako mkononi unaposoma ujumbe huu Soma kila andiko la biblia ambalo limeonyeshwa ili uweze kuelewa vizuri  

Yesu alisema, “ … nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda – Mat 16:18”. Je kwa kusema kanisa, alimaanisha nini?. Ni mjengo – yaani nyumba, ama ni kundi la watu? Na kama ni kundi la watu; ni watu wa aina gani? Leo tunaona nyumba nyingi zenye misalaba juu yake zinaitwa kanisa. Pia, tunaona, makundi makundi kila mahali kanisa la Yesu.

Neno “ kinisa”, ni tafsiri kutoka kwa neno la kigiriki- “Eklessa” maana yake ni walioitwa. Kufikia hapo, ni wazi kwamba sio mjengo mbali ni watu walioitwa. Kudhibitisha hayo Yesu alinena na mitume akiwaambia; “ … mbali mimi naliwachagua kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia – Yohana 15:19;17:14”. Kwa hivyo ni watu walichaguliwa kutoka ulimwenguni. Swala ni hili; watoke ulimwengu waende wapi? Eleweni jambo hili kwanza. Ulimwengu sio hii ardhi tunaoikalia, wala sio watu wanaoikaa. Ulimwengu ni aina ya maisha ambayo yalianzishwa na shetani (kitabu chetu kinachoitwa” CHANZO CHA UASI”  kina maelozo zaidi. Agiza utatumiwa). Wale wanaishi kulingana na hayo maisha wanaitwa walimwengu. Kwa hivyo kutoka ulimwengu ni kuyaacha hayo maisha na kufuata mengine

Basi je, watoke ulimwengini  (waache haya maisha) waende wapi? Waanzisha vikundi kama wanavyopendelea wenyewe ama wafuate nini? Ndiyo, Mungu katika kristo Yesu akimuita mtu huwa anampeleka wapi, ambapo anaenda kuwa sehemu ya kanisa lake?

Kanisa Limejengwa Juu Ya Neno La MunguMaandiko kutuambia kuwa kanisa la Mungu limejengwa, “ … juu ya msingi wa mitume na manabii, kristo mwenyewe akiwa jiwe la pembeni = Waeb 2:19-20. hii inamaanisha nini? Hebu tusikie maandiko yakijibu. “ Mungu … alisema na baba zetu kwa njia ya manabii.., mwishoni wa siku hizi anasema nasi katika mwana .. Waeb 1:1-2. yale maneno manabii na mitume waliongea, ni Mungu katika Yesu alikuwa akiongea ndani yao – ona 2Petro 1:19-201 yesu ndiye yule Mungu aliongea kwa manabii katika agano la kale. Tunajuaje? ( agiza ujumbe wetu huitwao “ YESU NI MUNGU NA NI MWANA WA MUNGU’) . kwa hivyo kujenga juu ya msingi wa mitume na manabii ni kujenga juu ya ile neno la Mungu waliyoiongea.   

BASI JE, UTOKE UENDE WAPI?

 Yesu anatujibu ; “ mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao sio wa uilmwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu – Yohana 17:14” . Yesu alikuja akitangaza habari za kuja kwa ufalme wa mugnu amboa, masha yake ndiyo yanaoelezwa na noeno lake katika biblia, kwa hivyo kutupa neno lake ni kutujulisha hayo maisha ya ufalme wa Mungu. Basi, wale wanaoyaacha maisha ya ulimwengu uitwa kuingia katika maisha ya Mungu. Hivyo basi, wanaotoka ulimwenguni ( maisha ya shetani) na kuenda ama, kuanza kuishi maisha ya Mungu wakiongozwa na neno lake – soma Zaburi 119:105, kwa uwezo wa roho mtakatifu; chochote kile wafanyacho katika maisha yao, huwa wanafanya kulingana na neno la Mungu.   

HUWEZI KUAMUA MWENYEWE KUJIUNGA NA KANISA LA MUNGU

 Najua wengi watashanga nikisema hivi. Lakini !! nasema ukweli ama ni kitu nimefikiria tu? Kumbuka, kweli ni neno la Mungu (Yohana 17:17). Basi je, naongea neno la Mungu ama filosofia ya wanadamu? Hebu tusikie yesu anavyosema. “ Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka … Yoh 6:44” . watu wengi ambao Mungu hajawavuta kwa Yesu, wamejifanya kuishi maisha ya Mungu na hii imezaa makundi yale unayoona leo ambayo yanatofautiana kuhusu ukweli wa Mungu. Yesu anazidi kueleza vile haiwezekani mtu kuelewa huu ukweli kama Mungu hajamfunulia. “ hakuna amjuaye mwana ila baba, wala hakuna amjuaye Baba ila mwana, na yeyote ambaye mana apenda kumfunulia – Luka 10:22”.  Umesikia isipokuwa yesu aamue kukufunulia haya maisha ya ufalme wa Mungu, huwezi kuyaelewa. Hivyo, huwezi kuyaishi ama kuyafuatia. Hii ndiyo sababu Yesu aliwaambia mitume (ambao sio wao walimchangua bali ni yeye aliwachagua) hivi;” … Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa- Mat13:11”  KANISA LA MUNGU NI LA WATEULE PEKE YAO  Usishangae eti tunawandikia ujumbe na kusambaza kadi tukiwauliza kama mnataka kuelewa hii injili ya Yesu, na huku tunasema ( na sio sisi tunasema ni biblia) kuwa mtu hawezi kuelewa kabla Mungu hajamfunulia. Ukweli nimkwamba, tunatii amri ya Bwana yesu kristo ya kuhubiri hii injili ya kuja  kwa ufalme wa Mungu hapa duniani, iwe ushuhuda kwa watu kabla mwisho haujaja. Ni wito tu kwa wale wachache ambao Mungu amewachagua katika kristo, ambao ndio wanaitwa wateule. Kwa vile hili neno hili tunalowaandikia sio letu, bali ni la Yesu, ikiwa wewe ni mmoja wa wateule, utaona  tu unaielewa na kuipenda maana ni sauti ya Yesu ambayo wote anaowaita wanaielewa  Alisema, kondood wake (wateule) wanaijua sauti yake  Yesu alipokuja duniani, maandiko iansema; “ulimwengu hawakumjua ijapokuwa ni yeye aliwaumba – Yoh 10:26-27; 1Yoh 4:6” kwa hivyo ni wale tu ambao Mungu amewaingiza katika hilo kanisa ambao wanaijua, kulikubali na kuyaelewa mafundisho yake. Wegine usema;” (soma – Mitume. 17:6;24:5-6; 25:7)’ .  Kwa hivyo wandugu, kanisa sio mjengo na wala sio kundi la watu waliofikiria kuungana tu; bali ni kundi la watu ambao Mungu mwenyewe aliwaunganisha kwa neno lake. Ni watu ambao Yesu Kristo amewapa uwezo wa kuelewa, na kulitii hili neno. Kuna tofauti kubwa sana kati ya hili kanisa la kweli na hay makundi ya ulimwengu yanayojiita makanisa. Kuna tofauti kati ya injili ya kweli ya yesu, inayohubiriwa na kanisa la kweli na, injili za uongo zinazohubiriwa na makundi yanayojiita kwa jina la Yesu ( soma 2 Timo4:3-4; Math 7:21). Unataka kutofautisha?. Agiza kitabu chetu kiitwacho, “ JE UTAIAMINI INJILI YA KWELI” . Swala la mwisho. Hili kanisa la kweli ni gani? Ikiwa unayo hamu ya kuelewa, ngojea ujumbe utakaofuata hivi karibuni.