KHOFH

NI YUPI MKUU NA WA KWANZA

NENO “MKUU” ina maana ya; kuzidi kiasi kwa idadi, kimo au hali.

Katika hiki kisasi, mtu huhesabiwa kuwa mkuu kulingana na kile alicho, kile afanyacho, na kile alicho nacho.

Mwenye elimu ya juu zaidi usemekana ndiye mkuu na aliye mbele kwa upande huo wa elimu. Mwenye nguvu zaidi, aliye tajiri zaidi, mkali zaidi, aliye zidi kwa mbio, na mengine mengi; hizi ndizo hali ambazo watu hutumia kupima ukuu wa mtu, ambaye usemekana kuongoza au kuwa wa mbele.

Wale wenye ukuu katika hizo hali, uheshimiwa, kuogopewa, kusikilizwa waongeapo, na hufuatwa. Wao pia hujivunia kuwa katika hizo hali, na uwadharau walio chini yao. Hivi ndivyo vipimo vya ulimwengu vya kuamua ukuu na uongozi, na vimekubalika.

Hii namna ya kuamua imefanya watu waanze kushindana, kung’angana, kubishana, ambovyo vimezaa chuki, vita na hata kuuwana.

Hali hii imeleta masengenyo, watu wakijaribu kuharibu wengine kwa maneno ya uongo huku wakijikweza wao wenyewe. Hii imefanya ushirikiano katika umma kuwa mgumu sana.

Je, hivi vipimo vya ulimwengu ni vya kweli? Eee, nauliza, huu ni ukuu na uongozi wa kweli? Ukuu na uongozi wa kweli unaweza kuleta chuki, vita na mgawanyiko katika umma?

Ni nani anaweza kulijibu hili swali?

ALIYE MWANZILISHI WA MAISHA

Kwa kutokuelewa, tunaweza kufanya mioyo yetu kuwa migumu, lakini ukweli ni kwamba, kunaye mmoja aliye muumba wa vitu vyote, ambaye Danieli alimnena hivi “ yupo mungu mbinguni afunuaye siri – Danieli 2:28,” na ndiye aliyapanga maisha. Yeye peke yake ndiye ajuaye ukuu na uongozi wa kweli.

Karibu miaka elfu mbili iliyopita, alimtuma mjumbe wake hapa duniani, yesu kristo ambaye, alikuja na kuwachagua wachache miongoni mwa wanadamu na kuwajulisha ule ukuu na uongozi wa kweli. Kitu cha kwanza, aliupinga huu mpango wa ulimwengu unaotumika kuamua aliye mkuu na wa kwanza.

Aliwaambia,

“ …. Msiwe Kama Ulimwengu Huu …

Katika kanisa la Mungu leo, ambalo ndilo hawa wachache waliafunuliwa huo ukweli, tunaona kila aina ya magombano na mizozano, huku watu waking’ang’ania ukuu na uongozi. Ajabu ni kwamba, wanatumia vile vipimo vya kiulimwengu na ndiyo sababu wanatofautiana, na kuzozana sawa na walimwengu.

Kile unachosoma hapa sasa hivi, ni sauti ya kipekee iliao nyikani (soma. Isaya 40:3), na inakukumbusha ule ukuu na uongozi wa kweli, kama uliyofundishwa na yesu mwenyewe.

Kwa hivyo, alisema aliye mkuu na wa kwanza ni mtu wa hali gani? Ni yule aliye zidi kiwango katika zile hali za kidunia, yaani, utajiri, nguvu, elimu, siaza, mbio nakadhalika?

Hebu tumsikilize yeye mwenyewe akitueleza. “ mwajua ya kuwa wakuu wa mataifa uwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu….” .Hebu tujaribu kuelewa tafadhali. Vitendo vyovyote watendavyo wakuu wa dunia si vizuri na hivyo, visionekane kwenu hata kidogo. Ndiyo, hatuwezi kujipanga na kuonyesha ukuu na uongozi kwa namna hii ya mataifa, vile wajionyeshavyo wakuu wa dunia. Ukitaka kuelewa ukuu wa kweli, hilo ndilo jambo la kwanza kuelewa. Baada ya hiyo, yesu anazidi kutueleza. “ … Bali, mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu yeyote atakaye kuwa wa  kwanza kwenu, na awe mtumwa wenu – Mat 20:25 –27”.

Elewa kama unaweza tafadhali. Aliye mkubwa ni mtumishi, atumikiaye wengine, na wa kwanza ni mtumwa, atumikaye kwa lazima, hata kinyume cha mapenzi yake.

Watu wakisoma hiki kifungu juu juu wamekosa kuelewa maana yake. Wale wanaohudumu kanisani kwa kueneza injili na kuwafundisha wengine, udhania eti, hiyo peke yake ndiyo maana ya utumishi, na hivyo ujionyesha kama viongozi na sio watumishi. Wengine huemda ele upande mwengine na kupinga kuwepo kwa uongozi wa yesu katika kanisa.

Je, yesu kristo anamaanisha nini katika hiki kifungu?

Hebu tusikilize maelezo ya neno baada ya nyingine ya hicho kfungu.

ALIYE MKUBWA NI MTIMISHI

Mtumishi ni mtu wa aina gani, ambaye ndiye jesu anasema kuwa nimkubwa kati yenu? Neno “mtumishi” inatokana na “utumishi”. Inamaanisha, kufanyia wengine kazi; kutendea wengine (sio wewe binafsi), kutumika kwa faida ya wengine. Kwa hivyo, mtumishi ni yule atumikaye kwa hiyo namna imeelezwa hapa. Sasa, ni utumishi gani mtu anapaswa kutumikia wengine ndani ya kanisa la Mungu ndio apate kuwa mkubwa zaidi ya wengine? Bwana wetu yesu kristo anasema; “ basi yoyote mtakayo tendewa na watu, watendeeni vivyo hivyo… Mat7:12”.

Huu ndio ule utumishi mtu anapaswa kutumikia wengine nao, ikiwa anataka kuwa mkubwa. Hivyo basi, nakuuliza; “ungependa watu wakufanyie nini?

Ni wasi tunapenda kupewa vitu, kufanyiwa kazi, kukubaliwa, kusifiwa, kuungwa mkono, kupendwa, kusamehewa na kadhalka. Chochote kizuri, tunapenda watu wakielekeze kwetu. Hivyo ndivyo tupendao watu watutendee.Ikiwa sasa hivi, bado tunataka watu watufanyie hivyo, basi, sisi si watumishi bali, ni wanaotumikiwa na hivyo, hatuwezi kuwa wakubwa katika kanisa, maana Bwana wetu amesema, mkubwa ni yule anayefanyia mwingine hivyo. Akiunga hilo jambo mkono, anasema; “… kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzake kuwa bora kuliko yeye binafsi. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine- wafilipi 2:2-4”.

Sasa hivi ndani ya kanisa, kila mtu anang’angania kutambulikana. Lakini yesu amekataa na kupinga hiyo tabia. Anasema kuwa, yule atakuwa mkubwa kwenu, ni yule atang’angania kutambua wengine, kuwaheshimu, kuwasamehe, kuwakubali (katika kweli); ndiyo, ni yule saa yote anatafuta kuwaelekezea wengine huo wema, akitafuta kuwapa, kuwafanyia kila wakati. Mkubwa ni yule ambaye audhiki watu wanapomdharau, au wanapokosa kumtambua, maana nia yake sio kuheshimwa au kutambuliwa na wengine bali, yeye utafuta kuwafanyia hivyo wengine. Hatarajii kutoka kwa wengine bali, yeye ujitahidi kuwapa wengine.

Mkubwa ni yule anafuata nyayo za yesu maana; “ … Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa nafisi yake iwe fidia kwa wengi – Mat20: 28”. Mtu anapokutukana, amekataa kukutumikia. Ukitaka kuwa mkubwa, huwezi kuanza kugombana na yeye, ukimrudishia matuzi, ili watu wajue wewe ni mkali pia. Bali, utamtumikia kwa; “ … tukitukanwa, twabariki; tukiudhiwa, twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kuwa takataka za dunia … 1 Wakorintho 4:12-13”

Ikiwa tunakumbuka maana ya neno “mkubwa au mkuu” yana maana ya, “ aliyezidi kiasi”, basi, tutaelewa kwamba ukubwa (ukuu) katika ukristo hauwi kwa kushinda wengine katika mabishano, huku ukijikweza mwenywe. Ni kwa kuzishika amri za mungu na kuzitenda ( kuziishi) kuzidi  wengi.

Ikiwa huu ndio ukubwa, mashindano yatatoka wapi na kila mtu anajitahidi huishi kulingana na maagizo ya Mungu, huku akitafuta kutambulikana na kukubalika  na Mungu mwenyewe? Jirani yako, au ndugu yako ataingilia wapi hapa, hata mjikute mnagombana?

Kitachokuwa katika ukubwa huu wa kweli ni, kila mtu kujitahidi kuishi kama yesu, na sio kung’ang’ania kutawala au kuongoza wengine. Hatutatafuti kutambulikana na wanadamu bali, na Mungu (soma 2 Wakorintho 1:17).

Aliye mkuu ni yule anayejitahidi kuishi kama yesu ambaye alijitahidi kuishi kama Mungu. Yesu mwenyewe anadhibitisha hayo akisema, “ iweni na nia yiyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwa ndani ya kristo  – Wafilip 2:5

Yesu alikuwa na nia gani? Hii inatuletakwenye sehemu ya pili ya jibu la yesu kuhusu aliye wa kwanza kwenye kifungu chetu.

WA KWANZA NI MTUMWA

Mtumwa ni mtu ambaye ni mali ya mtu mwingine.ni mtu ambaye humfanyia mtu wengine kazi kwa lazima.

Je mtu wa hali ya mtumwa, mtu wa kulazimishwa kutumikia wengine, kweli anaweza kuwa kiongozi? Kuwa wa  kwanza? Kwa mpango wa ulimwengu, haiwezekani. Lakini, hii hali ya utumwa ndiyo inayo mthibitisha mtu kuwa mkubwa na kiongozi katika kanisa la mungu. Tunawezaje kuwa watumwa kwa wengine? Bwana wetu anatuambia; “ Tena alikufa kwa ajili yetu ili waliohai, wasiwe hai tena kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa kwa ajili yao – 2 Wakorintho 5:15” na tene; “ … maana mlinunuliwa kwa thamana. Basi sasa, mtukuzeni mungu katika miili yenu – 1 Wakorintho 6:19-20”.Hapa, ni wasi kwamba, wale walio wa kanisa la mungu ni watumwa wa wanadamu ulimwenguni kwa anjili ya yesu.kwa njia gani? Tunaendelea kutoka ulimwenguni, kutoka kwa mapenzi ya mwili, yaani; ”… tamaa za mwili, tamaa za macho, na kiburi cha maisha – 1 Yohana 2:16”.  

Katika hayo maisha ya mwili, tunajitumikia sisi wenyewe; tunajitetea, tunajionyesha, tunatafuta faida zetu wenywe huku tukionyesha uwezo wetu wenyewe mbele ya wanadamu wenzetu.Mtu akichukua kitu chetu, tunamdai kwa lazima, kwa fujo, hata kumpiga ili tusiadhaniwe kuwa waoga au wanyonge. Tunaonya na kutoa tisho. Haya yote ni kwa kuonyesha na kutafuta utukufu mbele ya wanadamu- ukuu wa ulimwengu. Lakini sasa, yesu amebadilisha hayo na kusema; “… mtu yeyote akitaka kunifuata (kuwa wa kwanza) na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, na anifuate – Marko 8:34-35.”Hapa ndipo utumwa unaingilia. Ijapokuwa, inaweza kuwa haki yako kutenda jambo fulani; kama kudai mali yako kwa jirani yako, kutukana ukitukanwa, kuaibisha unapoaibishwa, hufanyi hivyo.  

Mbali na hayo, unatenda vile Mungu amekuagiza, (hata kama, kwa kutenda hayo, utaonekana, mnyonge, mjinga au mwoga) ili maisha ya yesu yasomwe ndani yako, hivyo kumuiga yeye, maana, “yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye haki- 1Petro2: 23”. “ … Aliustahimili msalaba, akaidharau aibu … Waebrania12: 2”, akawa mtumwa maana hakutenda mapenzi yake, bali ya Mungu aliyemtuma. Hivi ndivyo yule wa kwanza, ambaye ni kiongozi ndani ya kanisa anapaswa kufanya. Hatuoni yesu popote pale, akitoa mfano wa kujisema yeye mwenyewe kujitetea au, kuvutia watu kwake. Aling’ang’ania kuishi na kuongea maisha ya Mungu. Aliyapoteza yale yake ili ya Mungu yaonekane.

Aliongoza kwa vitendo na sio kuamrisha tu. Aliamrisha kile alikuwa akitenda mwenyewe. Kulingana na hayo maelezo ya yesu, unajiona wewe kuwa mkubwa, na kujiita kiongozi?  Kama itakuwa kweli, ni lazima ujisahau na usahau dhamana yako mwenyewe ili dhamana ya yesu ionekane ndani yako. Ni lazima ufanye wema, hata wakati unafanyiwa ubaya wa kila aina.“ … Lakini, eleweni ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana – Waefeso5:17”

Nimetaja hiki kufungu maana wengine hufikiria kwamba, kutenda wema ni kushirikiana na watu katika mapenzi yao. Tuelewe hivi; ” … wema ni kutenda sheria za Mungu – Warumi7:12”.

Kwa hivyo, huu utumwa unahusisha, kule kukaa maisha ya upweke (bila marafiki) ikiwa hiyo ndiyo inatakiwa ili tutende mapenzi ya Mungu. Ni kawaida kutaka kushirikiana na wengine, hata kuungwa mkono na wengine. Lakini kama hiyo inatufanya tuvunje sheria za Mungu, tunakaa peke yetu.

Tunakuwa watumwa maana kulingana na mapenzi yetu, tungeshirikiana na watu na, kufurahia kuungwa mkono na wao. Lakini tunapoteza hayo yote, hata kukubali kunyimwa haki yetu, ili tumtumikie bwana, na kuyaonyesha kwa hawa wanaotuchukia,

Hivi ndivyo tunakuwa watumwa, na ndiyo inayomchukuwa mtu kuwa wa kwanza, kiongozi. Huku ndiko kuwa mkubwa na kiongozi ama, wa kwanza katika kanisa ya Mungu.

WATAKA KUONGOZA?

Bwana wetu na mwokozi utuambia “… mtu akitamani kazi ya askofu (kiongozi), atamani kazi njema- 1Timotheyo 3:1 “Yesu hasemi kuwa ni vibaya kutaka kuwa mkubwa na wa kwanza. Kwa nini? Maana ikiwa unaelewa ukubwa wa kweli, basi kwa kuutaka, utakuwa unataka kuishi maisha ya Mungu huku ukiwapa wengine nafasi (kuwaongoza) ya kuyaona ndani yako. Hii ndiyo sababu anauliza; “ ni nani aliye na hekima na ufahamu kati yenu… Yakobo3:13?’  Je wewe unajiona kuwa mwenye hekima na ufahamu kutushinda sisi zote (kuwa mkubwa)?

Je unajifikiria kuwa mwenye haki kupita kila mtu? Unajiona mwenye kufaa kuwa kiongozi wetu? Kama ndiyo, Bwana yesu anakuambia utatenda namna gani? Anakuambia utusukume hapa na pale, huku ukiamrisha na kutulazimisha tukutii, tusalimu amri zako? Ni tabia ya aina gani ambayo upaswa kutenda ili uwe kweli unatuongoza kwa yesu na ndani yake? (Kwa maelezo zaidi kuhusu uongozi kuhusiana na wanadamu, agiza ujumbe, “ YESU NDIYE KIONGOZI”).

Eee, ni uongozi wa aina gani unaokubalika na Mungu ambao ulifundishwa na yesu kristo? Hebu turudi kwenye kifungu chetu cha yakobo na kuona, kile yesu atatujibu juu ya hayo maswali.“Ni nani aliye na hekima kati yenu (anayejiona kuwa heri, kuwa kiongozi)? Na aonyeshe kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wenye hekima – Yakobo3:13”.

Wapi kule kusukuma, kuamrisha, kutisha na kuweka wengine chini yako? Hakuna. Kilicho hapa ni kutenda hicho unachojiona kufahamu zaidi ya wengine. Hapo hakuna mabishano, magombano, wala kung’ang’ania. Ni kuishi tu ili watu waona utakatifu na uhaki (maisha ya Mungu) wa kweli ndani yako.

Hapa, kunao kung’ang’ania kukubalika mbele ya Mungu na sio mbele ya wanadamu. Wenye magombano, masengenyo, kung’ang’ana na mambo kama hayo sio wa kanisa la Mungu na wala hawana sehemu katika utumishi wa yesu. Maana Mungu anainena hii tabia kuwa “Lakini, mkiwa na wivu, wenye uchungu, na ugomvi mioyoni mwenu… hekima hiyo… ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na shetani – Yakobo3: 14-15” washirika wote wa kanisa wanajifunza kuwa viongozi katika ulimwengu ujao, wakati yesu atarudi na kuimarisha ufalme wa Mungu hapa duniani. Kwa kila mmoja ambaye anaongozwa na roho wa Mungu, jambo la muhimu ni kuumbika uhaki na utakatifu ambao huja kwa kutenda kwa uangalifu, neno la Mungu, kwa maana, “ hii amri ndiyo hekima na ufahamu wenu- Kumbukumbu 4:6”. Yeye ambaye Mungu amempa kipawa cha uongozi miongoini mwetu, utumia hicho kipawa kujenga uhaki wake, na sio kuhakikisha kwamba kila mtu yuko chini yake. Hii ndiyo sababu paulo anasema, “Si kwamba tunatawala imani yenu; mbali tu wasaidizi wa furaha yenu –2 wakorintho 1:24”

Mshirika, katika kile kipawa chake, hafanyi bidii ili atambulikane na kiongzi, bali, anang’ang’ania kuwa mtakatifu, kujitahayarisha kwa ile karamu ya Bwana harusi ambayo imekaribia sana.

Kwa vile wote ni washirika na sehemu za mwili mmoja, kila sehemu inajitahidi kutimiza huduma yake, ili hizi kazi tofauti zikiunganishwa zilete kazi kamilifu. Hatujawahi kuona sehemu za mwili zikibishana. Hatujawahi kuona mkono ukitamani kazi ya mguu. Mbona sehemu za mwili wa yesu (kanisa) zinang’ang’ana? Wandugu , mtu akitaka kuwa mkubwa na kiongozi na amtii Mungu kuwa kutenda amri zake.

Na atumikie kipawa chake kama yeye asimamaye mbele ya Mungu, na sio mbele ya wanadamu. Ishi kama uko peke yako, ukisimama mbele ya Mungu, ukitimiza kusudi lake la kukuumba katika haya maisha ya kimwili ambayo ni kuumbika tabia yake Kuwa mkubwa na wa kwanza hakutegemei kung’ang’ana na ndugu yako na kumshinda kwa maneno. Hakutengemei kukubaliawa na kuungwa mkono na watu. Kunategemea kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.

Hivyo basi, ukitaka kutafuta wale Mungu amewapa kipawa cha uongozi, tafuta mtu mwenye tabia za namna hii imeelezwa kwa huu ujumbe. Tujue kwamba tumeitwa tufundishwe kuwa wakubwa na wa kwanza katika ufalme wa Mungu hapo yesu atakaporudi. Huwezi sikiliza watu na ukafurahi wanapokusema kuwa unafaa, ukitumia hiyo kama thibitisho kuwa wewe ni mkubwa, na mwenye haki. Mungu anatuambia “… mkimtazama yesu, mwenye kuanzisha na kutimiza imani yenu -Waebrania12:2” tutakuwa saa zote tunajibidiisha kukubaliwa na Mungu, huku tukijifananisha na yesu.

Tutamsikiliza mtu tu, ikiwa hako ndani ya yesu. Na tutamjua kuwa ndani ya yesu, ikiwa anatenda na kuongea maneno ya yesu. Ukubwa na uongozi wa Mungu hauna, mabishano, ugomvi, mng’ang’ano na vita vya aina hii.

Je, unataka kuwa mkubwa na wa kwanza?Unatamani kitu kizuri. Fanya yale yote yameelezwa kwa huu ujumbe, na ni nakuambia, kwamba utakua mtu wa kuwatia wandugu zako moyo badala ya kugombana nao maana imeandikwa; ”… unifahamishe nikajifunze maagizo yako. Wakuchao wataniona na kufurahi, kwa sababu nimelingojea neno lako:.” wakuchao na wanirudie, nao watazijua shuhuda zako – zaburi119:74,79”. Ndiyo, kwa sababu maisha yako yatakuwa ni yale ya Mungu na sio yale yako.

Mtu wa namna hii ndiye mkubwa na wa kwanza. Huyu ni yesu akikuzungumzia kupitia kwa SAUTI NYIKANI