KHOFH

WAKATI WA WOKOVU NDIO HUU PEKE YAKE. KWELI?  

Mungu alimuumba Adam akiwa mkamilifu kwa upande wa mwili na akili ya kimwili pia. Hii akili ya kimwili haiwezi kufahamu mambo ya kiroho ( 1. wakori2:14). Kwa hivyo, adamu alihitaji akili ya kihoro ili aweze kumfahamu Mungu na maisha yake. Mungu alipomweka Adamu na Eva katika edeni, aliwapatia nafasi ya kumpokea roho matakatifu ambayo uelezwa kwa njia ya” mti wa uzima – Mwa 2:9” kwa maelezo zaidi juu ya huu mti, agiza ujumbe uitwao,” CHANZO CHA UASI, utatumiwa.). je, adamu ni kwamba, walimpokea roho muovu ambaye uonyeshwa kwa njia ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya – soma. Mwa2:17; 3:4,6. mungu naye aliwatenga naye, akwakataza roho yake takatifu ( ona. Mwa 3:23-24), na kuwaachilia waifute waifuate hiyo njia waliojiamulia ambayo ni maish ya shetani.   MANADAMU HAKUMJUA MUNGU WALA MAISHA YAKE. Tangu hapo, Adamu na uzoa wake wote walitengwa na Mungu kama vile imeandikwa; “ sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe – Isaya 53: 6” tena; “… akili zao zimetiwa giza, nao wamefarakishwa na uzima wa Mungu … waef 4:14’. Hii ndio sababu Daudi anashuhudia akisema; “hakuna mwenye haki hata mmjoja. Hakuna afaamuye; hakuna amtafutaye bwana. Wote wamepotoka … Waru 3:10-12. ndigu zanguni, tangu hapo edeni, Mungu, maisha yake na neno lake ni vita vimefichika kama paulo anaposhuhudia akisema; “bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa … 1 wako 2:7”   

HATUA ZA WAKOVU

 Kile Mungu anachofanya katika mpango wa wokovu ulio katika kristo yesu, ni kufichua hayo maisha yake ambayo mwanadamu hakuyajua tangu mwanzo. Na hii anfanya kupitia  kwa kufunuliwa kwake mwokozi wetu Kristo Yesu …, na kuufunua uzima na kutokuharishwa kwa ile injili…. 2 Timo1:10”. Eee; injili ya Yesu inatangaza kuja kwa ufalme wa Mungu ambao ni wa kiroho, na wa milele. Ili tuweze kuurithi huo ufalme, ni lazima tupewe huo uzima wa milele, na miili ya kiroho isiyoweza kufa. Hii ndiyo sababu Paulo kwa hicho kifungu amesema; injili inafunua uzima na kutokuharibika. Swala kubwa ni hili: je, Mungu wakati huu, anawafunulia watu wote hii siri ya wokovu? Wengi, karibu wahubiri wote siku hizi wanafundisha kuwa wakati ni huu peke yake. Je, biblia nayo ambayo ni neno la Mungu, N ndio kweli, inasemaji, kuhusu mpango wa wokovu?.   HUU SIO WAKATI WA WOKOVU PEKE YAKE:     Yesu alipokuja aktangaza injili ya kuja kwa mealme wa mbinguni, wayahudi na hata waeuasi wake walidhania ataimarisha huo ufalme wake, wakati huo. Hapo ndipo bwana  wetu Yesu alianza kufafanuo huu mpango wa wokovu. Aliwapa mithali ya mutu tajiri(kabaila) aliye kwenda nchi ya mbali kujipatia ufalme kisha arudi. Akawaita wafanya kazi kumi baadhi ya watumwa wake. Akawapa mafungu kumi ya fedha huku akiwaangazia waifanyie biashara hadi atakaporudi.——. Ikiwa aliporudi baada ya kupata ufalme, aliwaita hao kumi ajue faida walioipata. Wa kwanza alizarisha mala kumi naye tajiri akampa mamlaka juu ya miji kumi aitawale— wa pili— na kadharika.(soma Luka 19:12-13,15-25).   SASA NI WAKATI WA WOKOVU KWA WATEULE PEKE YAO Huyo tajiri sio mwingine ila ni Yesu Kristo. Aliwaeleza wayahudi kuwa ufalme wa mbinguni hauji wakati huo. Yesu aliwaelezea kwa hiyo mithali, vile atarudi binguni kwanza akaapishwe(soma Daniel 7:13-14). Ukisoma vizuri Luka 19:13, utaona kwamba, Yesu hakuita watumwa wake wote bali aliita kumi baadhi yao. Maana yake nini? Wakati huu wa kwanza, yesu hakuja kuita kila mtu; aliita wachache ambao ndio wanaitwa wateule na akawapa roho yake takatifu (mfano wa fedha katika mithali). Kwa vile Mungu, maisha yake, na hata neno lake ni roho, ni lazima mtu ampokee roho mtakatifu ili kumfahamu Mungu, na hivyo, kumwamini. Kwa hivyo, hao aliowaita, aliwapa roho mtakatifu ili kumfahamu Mungu, na hivyo, kumwamini. kwa hivyo, hoa aliowaita, aliwapa roho mtakatifu, hii ikiwa ni njia ya kuwapa nafasi ya kuuendea mti wa uzima ambao watu walitengwa nayo tangu wakati wa Adamu (soma ufu 22:14; Mithali 3:18). Ni hawa wateule peke yao amboa kwa sasa, wamepewa nafasi ya wokovu. Ni wao ambao wamepewa ufahamu wa Mungu na maisha yake ambayo ni siri kwa ulimwengu wote (ona. 1 wakor. 2: 8-10). Hii ndiyo sababu walipomuuliza yesu kuhusu hawa watu wengine, aliwajibu;” … ninyi mmejaliwa kuzijua sisri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa- Mat 13: 10-11”. Hawa ndio wanaitwa kanisa ama nyumba ya mungu ( agiza ujumbe juu ya” KANISA NI NINI?) ambao kwao; … hukumu inaendelea (soma 1petro 4:17). Lakini Mungu kwa sasa hajaanza kuhukumu ulimwengu yaani, hajaanza kutoa wokovu kwa wote. Basi, kwa hawa wachache, na ikiwa wewe ni mmoja wao,ambao ndio wanaweza kuiewa biblia peke yao, maandiko yanawaambia, … tazama wakati uliokubalika ndio huu, tazama siku ya wokovu ndio  sasa – 2 wakor6:2” . hii ni kwa sababu, hili ni neno la kiroho na sio ya kimwili. Kwa hivyo, inaweza kueleweka tu kwa njia ya kiroho. Paulo akishuhudia hiyo alisema; “ nayo twanena … tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni- 1wakor2:13-14” ndungu zanguni, kama mnataka ukweli, hii ndiyo hatua ya kwanza ya wokovu ambayo ni kwa wachache.    

WAKATI WA ULIMWENGU WOTE, NI ATAKAPOKUJA YESU

 Maandiko imetuambia kuwa hukumu inaendelea kwa wateule – kanisa la Mungu. Wanahukumiwa kwa njia gani, na ni kwa sababu gani? Maandiko yanasema;” kristo anatakaza kanisa (wateule), na kulisafisha kwa maji (roho mtakatifu) katika neno … waef. 5: 25-27” roho mtakatifu ni akili ya Mungu. Neno takatifu katika biblia ni hiyo roho katika maandishi (Yohana 6:63). Kwa uwezo wa roho mtakatifu, tunapoisoma neno la Mngu, inatuonyesha dhambi zetu (War 3:20; Yakobo, 1:23-25. sisi sote tunajua kuwa mashahara wa dhambi ni kifo- Warumi 6:23. kwa vile tukijiangalia kwa hiyo kioo ya Mungu – yaani, neno lake; tutana vile dhambi zetu zilivyo nyingi, kwa wale tunatubu, tuna zikubali. Sasa badala ya kuhukumiwa kifo, Yesu anaingilia hapo na kusema kwamba alikufa kwa niaba yetu na hivyo tunapata msamaha, ikiwa tu, tutawacha dhambi na kutii neno la Mungu ambayo ni amri zake. Hivyo mungu katika kristo anaendela kulihukumu kanisa ( Acts. 26:18) . kwa hivyo, wateule wanafundishwa kuishi maisha ya Mungu . Ya nini?.   WATEULE WATAHUKUMU (KUFUNDISHA) ULIMWENGU  

Tukirundi kwa ile mithali yetu, tunaona kwamba, yesu atakaporudi, atawapa wateule mamlaka juu ya miji ya dunia hii ili waitawale. Aliwaambia; nami nawawekea ninyi  ufalme… na kuketi katika viti vya enzi mkiwahukumu .. Luk 22:29-30”. Yesu aliendelea kuwaahidi; “ na yeye ashindaye nitampa mamlaka juu ya mataifa … Ufu 2:26-27”.Maandiko yanaendelea kusema kwamba Yesu; “amewafanya (wateule) kuwa ufalme na makuhani … nao wanamiliki juu ya nchi – Ufunuo 5:10”. Ndungu zangu, sio kwamba hawa wateule ni wema kushinda watu wengine lakini ni vile Mungu amewachagua mbele ili awatayarishe, kusudi, yesu ajapo kaitawala dunia, awatumie kuhumu ulimwengu. Paulo akijua hayo , alinena hivi;” au hamjui ya kuwa watakatifu watahukumu ulimwengu- 1Wakor6:3?  

Atakapokuja Yesu ataketi katika kiti chake cha enzi  na wateule pamoja naye (at25:31; Ufu 3:21) siku hiyo, mataifa yote ya dunia yatakusanyika mbele zake (Mat25:32). Shetani yule ambaye amekuwa akiwandanganya atatupwa kuzimu na kufungiwa miaka elfu mmoja. Kwa hiyo miaka elfu, kristo na wateule wataitawala dunia hii- Ufu. 20:3-6; Zekar14:9. hii ndio hatua ya pili ya wokovu ambao itakuwa ni kwa ulimwengu wote. Kwa miaka elfu moja, kristo pamoja na wateule watawatawala mataifa yote ya dunia na kuwahubiria neno lake. ( soma Isay 2:1-4); zaburi 22:27-31).

WALIOKUFA KABLA YA KUPATA NAFASI WAFUFULIWA

 Baada ya miaka elfu moja, shetani ataachiliwa. Na anaonekana akiwadangany’a baadhi ya wengi wa hao ambao wamehubiriwa kwa hiyo miaka yote. Atawongoza katika jaribio lake la mwisho la kuutega ufalme wa Mungu katika huo mji wa Jerusalemu. Watakapouzingira huo nji, kambi ya watakatifu hapo ndipo utashuka kutoka mbinguni na kuwamaliza. Hili ndilo ziwa la moto ( soma Ufu20:7-11). Kufikia hapo wanadamu wote wa kimwili watakuwa wamekwisha. Hayo yakiisha fanyika, tunaona kiti cha enzi, ambacho mbele yake, wanasimama wafu, wandogo kwa wakubwa. Wao wako katika mwili. Hapo nao pia watahukumiwa kwa miaka mia moja (soma Ufu 20:12; isay 65:19-22) . watakaotubu, watajiunga na wateule wenzao. Watakaoshindwa watatupwa kwenye ziwa la moto. Huu ndio utakuwa mwisho wa mpango wa Mungu wa wokovu kwa ajili ya Mwanadamu. Uovu wote utakuwa umekomeshwa; mbingu mpya na nchi mpya zitaonekana. Mji mpya yerusalemu utateremka pamoja na Mungu baba, na milele utaanza. Haya ndiyo mafundisho ya kweli kutoka kwa biblia. Kwa hivyo huu sio wakati wa wokovu pepe yake. Tujihadhari na manabii wa uongo na tuanze kujisomea biblia kwa maombi makuu ili tupate kutofautisha kati ya kweli na uongo.  wote wa kimwili watakuwa wamekwisha.